Na Mwandishi wetu, Blogu  ya Jamii
Katika kukuza Tanzania ya viwanda na kuleta ongezeko kwa  pato la nchi, Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) maarufu kama KONYAGI imezindua mvinyo mpya Valeur fortified white wine kwa wateja wake ambao unapatikana kwenye chupa yenye ujazo wa Milimita 200.

Uzalishaji wa Valeur fortified white wine  ni mojawapo ya mikakati ya kampuni hiyo ya kulipanua soko la zabibu jijini Dodoma na hivyo kuwaongezea wakulima wa zao hilo kipato. Mkoa wa Dodoma ni sehemu pekee duniani yenye misimu miwili ya zabibu kwa mwaka hivyo, una fursa ya kipekee ya kutumia zao hilo kutengeneza bidhaa mbalimbali.

Akizungumza katika uzinduzi wa kinywaji hicho kipya uliofanyika katika ofisi za TDL, jijini Dar es Salaam,  Meneja masoko wa kampuni hiyo Isaria Kilewo, amesema “Najivunia kampuni yangu inajivunia kuzindua kinywaji kingine kipya Valeur fortified white wine cha mvinyo na  ambacho kimetengenezwa kwa  kiwango cha hali ya juu na kinapatikana kwa bei nafuu. Mvinyo huu wenye harufu ya kuvutia, ukiwa na ubaridi ya nyuzi joto 18”amesema Kiwelo

Aidha, Meneja wa mauzo na usambazaji wa TDL Kanda ya Kusini Mwesige Mchuruza amesema, uzinduzi wa kinywaji hicho utafuatiwa na promosheni kabambe ya uonjeshaji ambayo itaanzia jijini Dar es Salaam tarehe 4 Oktoba mwaka huu ambapo pia utahusisha mikoa ya Morogoro, Dodoma, Arusha na Kilimanjaro.
 Meneja masoko wa  Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) maarufu kama KONYAGI Isaria Kilewo akizungumza na waandishi wa habari wakati uzinduzi wa kinywaji kingine kipya Valeur fortified white wine. Kulia ni Meneja wa mauzo na usambazaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) maarufu kama KONYAGI Kanda ya Kusini Mwesige Mchuruza.
 Meneja wa mauzo na usambazaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) maarufu kama KONYAGI Kanda ya Kusini Mwesige Mchuruza akizungumza na waandishi wa habari wakati uzinduzi wa kinywaji kingine kipya Valeur fortified white wine. Kushoto ni Meneja masoko wa  Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) maarufu kama KONYAGI Isaria Kilewo
Meneja masoko wa  Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) maarufu kama KONYAGI Isaria Kilewo(kushoto),  Meneja wa mauzo na usambazaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) maarufu kama KONYAGI Kanda ya Kusini Mwesige Mchuruza (kulia) pamoja na Warda Obeng wakionesha kinwaji icho kilichoziduliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...