MAMA, Leo hii unatimiza miaka tisa (9) tokea ulipotuacha hapa duniani. Kila siku tunakukumbuka Mama. Umetufundisha kukua katika upendo, ukweli, uaminifu na kumcha Mungu. Tunamuomba Baba  Mungu atuwezeshe tuyaendeleze na kuyaenzi mema yote uliyotufundisha na tuyaendeleze kwa vizazi vyetu vijavyo. MAMA, daima tutaendelea kujivunia zawadi tuliyopewa na Baba Mungu ya maisha yako kwetu sisi kwa maana uliyagusa maisha yetu kwa njia ya pekee.

Unakumbukwa daima na mume wako mpenzi Mzee Lawrence Shelukindo Saguti, watoto, wakwe na wakamwana, wajukuu na vilembwe

...........Tunaendelea kusimama imara na neno toka Ufunuo wa Yohana 12: 11
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.

..........Na tukimsifu Mungu tukiimba:
Amini Bwana awapenda, Amini,atawabariki, Atawahurumia wote, wamjiao yeye.
Kweli tutaona furaha, Tukifika kwenye Raha kuu, Tukisafishwa mioyo yetu na Yesu Mwokozi.


Endelea kupumzika kwa amani MAMA!


AMEN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hakika miaka mingi imepita kumbe tayari miaka 9 Mungu azidi kuwabariki na muendelee kumtumikia yeye, Familia yetu itamkumbuka sana Marehemu Mama Saguti. Apumzike kwa Amani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...