KESI ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake halali, inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai na wenzake wanne, imeshindwa kuendelea kusikilizwa sababu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina hela ya kuwaleta mashahidi.
Wakili wa Serikali, Pius Hila akisaidiana na wakili kutoka Takukuru, Vitalis Peter ameeleza hayo, leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.
Wakili Hilla amedai walishaita mashihidi kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam lakini wameshindwa kufika kwa kuwa Mtendaji wa Mahakama hakuwa na fungu la fedha, kwa ajili ya kuwalipa.Ameendela kueleza kwa sasa wamepata kibali kutoka kwa Mtendaji wa Mahakama ambacho kinawaelezea kuwa malipo yatasubiri fedha zitakapoingia lakini mashahidi wameshindwa kuja kwa gharama zao wenyewe.
"Mheshimiwa hakimu kutokana na hali hiyo, tunaomba terehe fupi kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi hii," ameeleza Hilla.Kutokana na maelezo hayo, Wakili wa Utetezi Alex Mgongolwa aliwasilisha maombi mawili mahakamani hapo.
,"Mheshimwa, tunaomba jitihada za kuwapata mashahidi hao waliopo nje ya mkoa wa Dar rs Salaam ziendelee na pia ni rai yetu kwa mahakama upande wa mashtaka walete mashahidi ambao hawahitaji kuombewa kibali na hawatoki nje ya mkoa wa Dar es salaam ili Kesi hii iweze kuendelea," amedai Wakili Mgongolwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...