BENKI ya NMB imetoa msaada wa mahema maalum pamoja
na fulana zitakazotumiwa na Taasisi ya Suleman Kova Security and
Disaster Management Foundation-Sukos-DMF wakati inazunguka kwa jamii
kutoa elimu namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali pindi
yanapotekea. Vifaa hivyo ambavyo ni mahema maalum nane pamoja na fulana
zitakuwa zikitumiwa siku ya tarehe 6 Octoba ikiwa ni siku maalumu kabisa
ya kuadhimisha siku ya maafa /majanga duniani.
Akizungumza katika tukio hilo la kukabidhi msaada huo, Meneja Mradi, Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB, Lilian Kisamba alisema tukio hilo ni mwendelezo wa benki hiyo katika kuisaidia jamii hivyo wanatambua na kuguswa na majanga na maafa yanayowakumba wananchi ambao ni jamii wanaoihudumia.
"Ni ada yetu NMB kuisaidia jamii inayotuzunguka kupitia kitengo maalumu cha CSR...tumekuwa tukifanya hivi maeneo mbalimbali..hususani sekta ya elimu, afya na huduma nyingine muhimu kwa jamii. NMB inaamini msaada huu utatasidia jamii kupatiwa elimu ya kujikinga na majanga unaweza kupunguza athari ya majanga hayo hata yanapotokea," alisema Bi. Lilian Kisamba alipokuwa akikabidhi msaada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Sukos-DMF, Suleiman Kova.
Alisema NMB itaendelea kuisaidia jamii katika maeneo mbalimbali kwa kuwa hakuna maendeleo ya kiuchumi pasipo na jamii salama na pia hakuna biashara inayoweza kufanya vema pasipo na jamii salama. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Sukos-DMF, Suleiman Kova (Kamanda mstaafu wa Jeshi la Polisi) alisema taasisi yake ya Sukos-DMF kwa kushirikiana na Benki ya NMB na wadau wengine imepanga kufanya uzinduzi wa mahema maalum ambayo yatakuwa yakitumika katika shughuli za kutoa hifadhi kwa wahanga wakati yanapotokea maafa.
Alisema zoezi hilo litakwenda sambamba na washiriki kufanya mazoezi (jogging) kuanzia eneo la uwanja wa taifa kuelekea viwanja vya Kituo cha Vijana cha Jakaya Kikwete na pia kutakuwa na tukio la washiriki kuchangia damu kwa ajili ya wahitaji, huku akisisitiza elimu ya kukabiliana na majanga kwa taasisi hiyo utakuwa ni mradi endelevu.
Meneja Mradi, Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB, Lilian Kisamba (wa pili kuklia) akizungumza na wanahabari kabla ya kukabidhi mahema nane ambayo yatolewa na NMB ambayo yatatumiwa na taasisi hiyo wakati inazunguka kwa jamii kutoa elimu namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali pindi yanapotekea.
Meneja Mradi, Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB, Lilian Kisamba (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Suleman Kova Security and Disaster Management Foundation, Sukos-DMF, Bw. Suleiman Kova (Kamanda mstaafu wa Jeshi la Polisi) moja ya fulana zilizotolewa na NMB kwa ajili ya Sukos-DMF.
Meneja Mradi, Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB, Lilian Kisamba (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Suleman Kova Security and Disaster Management Foundation, Sukos-DMF, Bw. Suleiman Kova (Kamanda mstaafu wa Jeshi la Polisi) moja ya fulana zilizotolewa na NMB kwa ajili ya Sukos-DMF.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Suleman Kova Security and Disaster Management Foundation, Sukos-DMF, Bw. Suleiman Kova (wa pili kulia) akizungumzia taasisi yake inavyofanya kazi zake kabla ya kupokeaa msaada huo toka NMB. Kutoka kushoto ni Msanii wa uigizaji, Salim Ahmad 'Gabo', Meneja Mwajiri wa Cops Security (T) Ltd, Ibraahim Mcherecheta na Meneja Mradi, Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB, Lilian Kisamba (wa kwanza kulia).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...