Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji nchini (TIC), Bw. Geoffrey Mwambe (aliyenyoosha mkono
ukutani), wakati akipata ufafanuzi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati)
na Mkurugenzi wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), Bw. Paul Rwegasha kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Tatu la
abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA-TBIII).

Mafundi (kulia juu ya mashine)
wakiwa wanaendelea na ujenzi wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, wakati wa ziara ya Wakurugenzi
wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela na
wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bw.Geoffrey Mwambe pamoja na
msafara wao, leo walipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi huo.

Mhandisi Barton Komba wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) anayesimamia mradi wa ujenzi wa Jengo la
Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA-TBIII), akielekeza jambo wakati wa ziara ya Wakurugenzi kutoka
Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bw. Geoffrey Mwambe (wapili kushoto)
na wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela
(watatu kulia) leo walipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya mradi
huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Uwekezaji nchini (TIC), Bw. Geoffrey Mwambe (alinyoosha mikono) leo
akijaribu kueleza kwa vitendo katika ziara yake aliyoambatana na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.
Richard Mayongela (watatu kushoto) walipotembelea ujenzi wa mradi
unaoendelea wa Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere, tayari ujenzi umefikia asilimia 82.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...