Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeombwa kusaidia uzalishaji wa zao
la chai wilayani Lushoto mkoani Tanga ili kuchagiza shughuli za kiuchumi
na kunyanyua kipato cha wakulima wadogo wadogo wilayani humo humo.
Ombi hilo
limetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. January Lugangika wakati
akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine
alipotembelea Ofisini kwake.
Bw. Lugangika
alisema kuwa Serikali imejipambanua katika kukufua viwanda hasa vyenye
kusaidia wakulima wadogo wadogo kupitia ununuzi wa malighafi akilitaja
zao la chai kuwa ni la kipaumbele katika kuchagiza juhudi hizo za
Serikali.“Benki ya Kilimo
ikisaidia kufufua viwanda vyetu vya chai itawanufaisha wakulima wetu
wanaolima chai hivyo kuweza kunyanyua kipato cha wakulima wilayani
kwetu,” alisema.
Aliongeza kuwa
wilaya ya Lushoto imejaliwa kuwa na eneo kubwa la uzalishaji zao la chai
hivyo kuongeza tija katika kuendeleza zao hilo.Akizungumza
wakati wa kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet
Justine alisema TADB ipo tayari kuchagiza uzalishaji wa mazao ya
kimkakati yenye masoko ya uhakika ikiwemo zao la chai na yenye kulenga
kunyanyua hali za maisha ya wakulima wadogo wadogo nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Bw. January Lugangika (wapili kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ulipomtembelea Ofisini kwake wilayani Lushoto kuzungumzia fursa za uwekezaji katika kilimo. Wanaomsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto), wengine ni Afisa Biashara Mwandamizi wa TADB, Eunice Mbando (kulia) na Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo, Bw. Tito Kayugyuma (wapili kulia).

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Bw. January Lugangika akihimiza jambo wakati wa kikao.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akifafanua jambo wakati akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Bw. January Lugangika (hayupo pichani).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akiwa katika mazungumzo na Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto, Bw. Nicodemas Tambo (katikati). Anayesikiliza ni Afisa Ushirika wa Wilaya hiyo, Bw. Tito Kayugyuma (kushoto).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...