NA LUSUNGU HELELA- SONGWE
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga ameanza ziara ya kimkakati ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini lengo likiwa ni kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao kwa wanafunzi hao.
Mhe. Hasunga amesema sekta ya utalii inaweza kuongeza pato lake maradufu iwapo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wataanza kujua umuhimu juu ya utalii wa ndani bado angali wakiwa wadogo.
Katika ziara hiyo aliyoianza mkoani Songwe wilayani Mbozi, Naibu Waziri Mhe. Hasunga ameweza kutembelea shule za Sekondari tatu ikiwemo Shule ya Kilimampimbi, Vwawa pamoja na Ilolo ambapo amezungumza na wanafunzi pamoja na walimu kuhusu umuhimu wa utalii wa ndani.
Amefafanua kuwa Wanafunzi ni mabalozi wakubwa wa mabadiliko, wanapopata elimu juu ya utalii wa ndani wataweza kuifikisha kwa wazazi, walezi pamoja na jamii kwa ujumla.
Katika ziara hiyo, Mhe. Hasunga ametoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliokuwa wakijibu maswali kuhusiana na vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Amesema sekta ya utalii inachangia asilimia 17.5 ya pato la taifa na inaweza ikawa asilimia 30 kama kutajengeka utamaduni kwa jamii wakiwa bado wanafunzi kuhusu umuhimu wa kutenga muda pamoja na pesa kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
‘’Nchi yetu imejaliwa kuwa na vivutio vingi lakini imekuwa haifanyi vizuri ukilinganisha na nchi kama Misri aambao wao hawana vivutio vingi kama tulivyonavyo sisi, Wenzetu wana magofu pekee lakini wametuacha mbali’’ amesema Mhe. Hasunga.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kilimampimbi iliyopo wilaya ya Mbozi
mkoani Songwe akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya
utalii vilivyopo nchini kwa lengo la kuongeza mapato yatokanayo na
utalii pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao.
Baadhi ya wanafunzi wa Vwawa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Vwawa iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani
Songwe akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii
vilivyopo nchini kwa lengo la kuongeza mapato yatokanayo na utalii
pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (katikati)
akizungumza na walimu wa shule ya sekondari ya Vwawa iliyopo wilaya ya
Mbozi mkoani Songwe mara baada ya kumaliza kuzungumza na wanafunzi
wa shuke hiyo kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo
nchini kwa lengo la kuongeza mapato yatokanayo na utalii pamoja na
kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilolo iliyopo wilaya ya Mbozi mkoani
Songwe akiwahamasisha kuhusu umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii
vilivyopo nchini kwa lengo la kuongeza mapato yatokanayo na utalii
pamoja na kukuza uzalendo wa kupenda na kuthamini vitu vya kwao
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akiwa na Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbozi, Bi. Hossana Mshule wakati w
akielekea kukagua baadhi ya majengo yaliyojengwa kwa mfuko wa jimbo la
Vwawa.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...