Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amekutana na kufanya mazungumzo na  waandishi wa habari za michezo ambapo wametumia muda mwingi kujadili mwenendo wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA).

Akizungumza na Waandishi hao, Dkt. Mwakyembe ameliagiza Baraza la Michezo nchini (BMT) kusimamisha Uchaguzi wa TASWA unaotarajiwa kufanyika Novemba ya mwaka huu.

Dkt. Mwakyembe ameiagiza BMT kuita uongozi wa TASWA na Uongozi wa Vijana ambao hawana Uanachama wa Chama hicho kukaa pamoja kujadiliana changamoto zinazokikabili Chama hicho.

"Uchaguzi wa TASWA usimamishwe na mkae pamoja mzungumze kuhusu Katiba ya Chama hicho ili baadae mpate uongozi ulio imara kwa maslahi ya waandishi wa habari za michezo nchini", amesema Dkt. Mwakyembe.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwakyembe amesema Wizara yake iko katika mikakati yakuboresha mazingira, ikiwa kuhakikisha kila .wandishi anakuwa na Bima itakayomlinda katika mslahi yake.

Pia kuunda Baraza la Habari (Media Council), Chombo cha Idhibati, Kamati ya Malalamiko itakayokuwa na Mamlaka ya Mahakama pamoja na Mfuko wa Wanahabari kwa ajili ya Mafunzo kwa Wanahabari.

Kwa kukumbusha TASWA iliundwa mwaka 1977 chini ya Sheria za Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...