Na Chalila Kibuda, Golobu ya Ja Jamii
NDOA za utotoni zimeendelea kuwa kikwazo kwa
maendeleo ya mtoto wa kike ambapo takiwmu za hali ya watu na afya nchini kwa
mwaka 2015/2016 zinaonyesha asilimia 36 ya wanawake umri wa miaka 25-49 wamepata watoto kabla ya
kufikisha umri wa miaka 18.
Hayo aliyasema Mchumi na Mratibu wa Mpango kazi wa Kitaifa
wa kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto kutoka Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Seto Ojwando katika mdahalo
wa Wadau uliofanyika katika Chuo cha Ustawi Jamii jijini Dar es Salaam.
Amesema tafiti za afya na uzazi na
viashiria vya malaria TDHS 2015/2016 zinaonyesha kuwa mwanamke mmoja kati ya 10
wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamekeketwa
huku mikoa ambayo inaongoza katika ukeketaji huo ni Manyara asilimia 58, Dodoma asilimia 47, Arusha 41,
Mara asilimia 32 pamoja na Singida asilimia 41.
Ojwando amesema katika tafiti hiyo ya
TDHS ya 2015, 2016 Mikoa inayoongoza kwa
mimba za utotoni ni Katavi asilimia 45,Tabora asilimia 43, Dodoma asilimia 39,
Mara asilimia 37 pamoja na Singida asilimia 34.
Amesema kuwa nia ya kukuatana na
wadau pamoja na wasomi katika Chuo cha ustawi wa jamii ni sehemu ya utekelezaji
wa mapango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na mpango wa vietndo vya ukatili dhidi ya
watoto ulianza 2017 ikiwa ni lengo
kupunguza vitendo vya aina zote ukatili dhidi ya mwanamke na watoto kwa
asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa
Jamii Dkt. Zena Mabeyo akifungua madahalo wa kitaifa wa kutokomeza ukeketaji
,Mimba na Ndoa za Utotoni uliofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mhadhili wa Chuo cha Ustawi wa
Jamii, Leah Omary akitoa mada katika madahalo wa kitaifa wa kutokomeza
ukeketaji ,Mimba na Ndoa za Utotoni uliofanyika katika Chuo hicho jijini Dar es
Salaam.
Mchumi na Mratibu wa Mpango kazi
wa Kitaifa wa kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto kutoka
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Seto Ojwando
akizungumza katika mdahalo wa kuhusiana na seriakli kuchukua hatua mimba za
utotoni, ndoa z utotoni pamoja na ukeketaji
Mhadhili wa Chuo cha Ustawi wa
Jamii, Zachayo Shigongo akitoa maada kusiana na malezi ya watoto katika madahalo
wa kitaifa wa kutokomeza ukeketaji ,Mimba na Ndoa za Utotoni uliofanyika katika
Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau katika mdahalo huo
wa kujadili na kutokomeza ukeketaji ,Mimba na Ndoa za Utotoni uliofanyika
katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...