Na Mwamvua Mwinyi,MKURANGA
SERIKALI Mkoani Pwani, imetoa onyo kwa watu ama vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS ) wanaoshawishi wakulima kukataa mfumo wa stakabadhi ghalani pamoja na kupeleka korosho kwenye maghala makubwa na badala yake wanawarubuni kuuza kwa mtindo wa kangomba .
Aidha umetoa wito ,kwa wadau mbalimbali kujenga ghala la Kibiti ili yaweze kupewa leseni ya kutumika katika msimu ujao wa ukusanyaji na ununuzi wa korosho .Akifungua mkutano wa wadau wa zao la kibiashara la korosho ,wilayani Mkuranga ,mkuu wa mkoa huo ,mhandisi Evarist Ndikilo alisema ,yeyote aliyejipanga kukataa mfumo huo ni mhujumu uchumi na biashara hiyo haikubaliki.
Alisema, kuwa na maghala machache ni mpango wa serikali hivyo hawatakuwa na nafasi ya kutumia maghala ya vichochoroni ambayo yameshasababisha changamoto nyingi msimu uliopita ."Tunazijua Amcos ambazo zilitutia doa ,tuwajua majina na mipango wanayoyafanya ,nawataadhalisha kabisa ,hatutaki tuharibu sifa yetu tena "tutamnyakua mmoja baada ya mmoja "
Ndikilo pia alikemea, baadhi ya wanunuzi wa korosho waache kuhujumu uchumi kwa kushinda minada kisha kushindwa kulipia kwa wakati na makubaliano ya mkataba na kuanzia sasa hawatawachekea wanunuzi wa aina hiyo."Msimu huu unaokuja hatutaki utani ,tumechoka kuwa kichwa cha wendawazimu ,kila mmoja anufaike mnunuzi na mkulima bila kumyanyasa mkulima " alibainisha.
Alielezea ,tangu wameanza kutumia mfumo huo msimu wa mwaka 2015/2016 waliuza tani 8,800 ,mwaka 2016/2017 tani 13,300 na msimu wa 2017/2018 tani 20,650 hivyo kila msimu umekwenda ukiongezeka kwa uzalishaji.
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo akifungua mkutano wa wadau wa zao la kibiashara la korosho ,wilayani Mkuranga.
Kaimu naibu mrajis -uthibiti kutoka tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania ,Collins Nyakunga akitolea ufafanuzi jambo wakati wa mkutano wa wadau wa zao la kibiashara la korosho ,wilayani Mkuranga ,mkoani Pwani.
Katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji ,Shangwe Twamala akizungumza jambo katika mkutano wa wadau wa zao la kibiashara la korosho ,wilayani Mkuranga ,Mkoani Pwani.
Baadhi ya washiriki kwenye mkutano wa wadau wa zao la kibiashara la korosho ,wilayani Mkuranga ,Mkoani Pwani .(picha na Mwamvua Mwinyi ).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...