Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

SERIKALI imewataka wafugaji nyuki nchini kuendesha ufugaji wao kwa njia za kisasa utakaowawezsha kuzalisha mazao yenye ubora na thamani kwa ajili ya kujiongezea kipato.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati wa maadhimisho ya siku ya kitaifa ya kutundika mizinga nchini iliyofanyika Novemba 03, 2018 Kalambo mkoani Rukwa katika shamba la nyuki Nawima lililopo katika Msitu wa Mto Kalambo.

Jumla ya mizinga 100 imetundikwa katika kuazimisha siku hiyo na kufanya idadi ya mizinga katika shamba hilo kufikia 362. Awali shamba hilo lilikuwa na mizinga 262 ikuhudumiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Hasunga amesema ufugaji nyuki ni fursa kwa vile mazao yake hutumika kama chakula na dawa lakini pia malighafi viwandani na soko lake la ndani na nje ni la uhakika ukilinganisha na bidhaa yoyote inayozalisha nchini.“Asali yetu inagombewa katika soko la dunia, muhimu kwetu kuzingatia uzalishaji wenye tija na kuacha tabia ya kukata miti na badala yake tulinde na kuhifadhi misitu yetu ambayo nyuki hutegemea katika uzalishaji wa mazao yake,” amesema Hasunga.

Kwa wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya ufugaji nyuki na kuwataka kuachana na shughuli za uchomaji mkaa na kujikita katika shughuli za kujiongezea kipato pasipo kuathiri misitu kama shughuli za ufugaji nyuki.Wakati huo huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo amewataka wananchi kuungana katika vikundi na kujenga viwanda vidogo vidogo na vikubwa katika maeneo mbalimbali ili Serikali iwasaidie.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Japhet Hasunga (kulia) akitundika mmoja kati ya mzinga 100 waliyotoa wakala wa huduma ya misitu (TFS) katika msitu wa Mto kalambo wenye Hekta 42,000.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kulia) baada ya kutundika mmoja wa mizinga ya nyuki 100 iliyogawiwa kwa vikundi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania(TFS)Profesa Dos Santos Silayo wa kwanza kushoto akishiriki kutundika mzinga wa nyuki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...