Na Margareth Chambiri.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imewaonya Wasimamizi wa Uchaguzi ambao ama kwa kujua au kwa makusudi wataharibu au kukiuka taratibu za Uchaguzi kutokana na kutofuata sheria na taratibu za Uchaguzi. 

Onyo hilo limetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi jijini Dodoma. 

Mheshimiwa Mbarouk ambaye amewataka Wasimamizi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea amesema Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na ile ya Serikali za Mitaa zinaunda kosa la jinai na kutoa masharti ya adhabu kwa Afisa yeyote wa Uchaguzi ambaye atasababisha kuharibu uchaguzi. 

Makamu Mwenyekiti huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema madhara ya kutozingatiwa kwa taratibu za Uchaguzi ni kusababisha kesi nyingi za Uchaguzi na kuitumbukiza Serikali katika gharama ambazo zingeweza kutumika katika shughuli nyingine za maendeleo. 

Amewataka Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kuyaelewa vyema maeneo wanayofanyia kazi na kujiamini ambapo pia amewakumbusha jukumu walilo nalo la kuimarisha imani ya wananchi na wadau wengine wa Uchaguzi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. 
Mkuu wa Idara ya Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Irene Kadushi, akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi. 
Mkuu wa Idara ya Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Emmanuel Kawishe akifafanua hoja katika mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi.
Afisa Uchaguzi Meshack Mgovano, akieleza jambo kwenye mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi.Picha zote na NEC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...