Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

VIJANA 7 wa umri wa miaka 21 hadi 24, leo wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kosa la kuharibu Noti za Benki Kuu ya Tanzania (B.O.T) za Shilingi 70,000 kwa kuzikanyaga.

Mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Vicent Kaduma (24), Rogers Swale (23 ), Doreen Mwenisongole (22) ni mwanafunzi, Kelvin Mngeyekwa 23, Eia Chengula 24 mfanyabiashara, Said Sadiq 21 na Ramadhan Seleman 23.

Akisoma hati ya mashtaka, chini ya kifungu cha 332 A cha kanuni ya adhabu, mbele ya Hakimu Mkazi Wanjah Hamza wakili Kombakono amedai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kosa moja la kuharibu noti za BoT.

Imedaiwa, Septemba 16 mwaka 2018 washtakiwa hao wakiwa jijini Dar es Salaam, pasipokuwa na mamlaka waliharibu noti za Sh.70,000 ambazo noti moja ilikuwa na thamani ya Sh. 10,000.Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo, washtakiwa hao wako nje kwa dhamana baada ya mahakama kupatiwa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini 2 waaminifu waliosaini bondi ya Shilingi Milioni 2 kila mmoja.  Kesi imeahirishwa hadi Novemba 11 mwaka 2018.
Pichani juu na chini ni baadhi ya watuhumiwa wakipandishwa kwenye kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kosa la kuharibu Noti za Benki Kuu ya Tanzania (B.O.T) za Shilingi 70,000 kwa kuzikanyaga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...