Dar es Salaam. Mwaka
huu unaweka alama ya maadhimisho ya miaka 10 ya Mbio za Rotary Dar,
tukio la hisani ambalo limekuwa likiweka rekodi kubwa katika usajili
kila mwaka.
Kupitia mbio hizo,miradi mbalimbali ya huduma za kijamii imekuwa ikitekelezwa kwa miaka tisa mfululizo iliyopita kupitia fedha ambazo huwa zinachangwa ikiwemo upandaji miti zaidi ya 26,000,utoaji wa huduma ya maji safi ya kunywa shuleni,
Ujenzi wa wodi ya saratani ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kituo cha maendeleo ya ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka huu, matembezi ya hisani na mbio za Rotary Dar zinalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa kliniki maalum katika Hospitali ya CCRBT itakayowezesha utoaji huduma na kupunguza gharama zinazotolewa kwa watu wenye ulemavu.
Mbio za Rotary Dar ni juhudi za pamoja baina ya klabu nane za Rotary jijini Dar es Salaam ambazo zimekuwa zikiungwa mkono kwa ufadhili mkubwa wa Benki M na Pepsi.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mwenyekiti wa Bodi wa Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt amesema, "Tunaamini ushirikiano wa kimkakati tuliokuwa nao na Benki M ulikuwa na mafanikio makubwa jambo lilopelekea muelekeo mzuri na kutoa motisha kwa wafadhili wengine katika ambao wanatuunga mkono mwaka huu," alieleza na kuongeza kuwa, "mwaka huu Pepsi nao wameongeza hatua nyingine zaidi kwa ajili ya kutangaza michezo Tanzania kwa kutoa ufadhili wa jumla kwa Mtanzania mwanaume na mwanamke atakayefanya vizuri katika mbio za kilomita 42.2, ambapo watapelekwa kushiriki mbio za Beirut Marathon nchini Lebanon.

Msanii
wa kike anayetamba zaidi nchini, Vanessa Mdee al-maarufu Vee-Money
ambaye pia ni Balozi wa wa Mbio za Rotary Dar kwa mwaka huu akizungumza
leo (Oktoba 02, 2018) jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kutangaza
rasmi maandalizi ya mbio za Rotary Dar zitakazofanyika Oktoba 14 mwaka
huu (Siku ya Mwalimu Nyerere). Vanessa atashiriki mbio za Rotary Dar kwa
mwaka huu lakini pia atatumia ushawishi alionao kuwahamasisha watu
wengi zaidi kushiriki. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa Bodi wa Mbio za
Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt (kulia) na Mkurugenzi Uendeshaji wa
CCBRT, Brenda Msangi (kushoto).
Mkurugenzi
Uendeshaji wa CCBRT, Brenda Msangi (kushoto) akionyesha kipeperushi kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo (Oktoba 02, 2018) jijini Dar
es Salaam kuelezea baadhi ya huduma maalumu zinazotolewa na hospitalini
hapo wakati wa hafla ya kutangaza rasmi maandalizi ya mbio za Rotary Dar
zitakazofanyika Oktoba 14 mwaka huu (Siku ya Mwalimu Nyerere). Pamoja
nae ni Msanii Vanessa Mdee al-maarufu Vee-Money (katikati) ambaye pia ni
Balozi wa wa Mbio za Rotary Dar kwa mwaka huu na Mwenyekiti wa Bodi wa
Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt (kulia).
Mwenyekiti
wa Bodi wa Mbio za Rotary Dar, Bi. Sharmila Bhatt (kulia) akizungumza
leo (Oktoba 02, 2018) jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kutangaza
rasmi maandalizi ya mbio za Rotary Dar zitakazofanyika Oktoba 14 mwaka
huu (Siku ya Mwalimu Nyerere). Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya
maandalizi ya mbio za Rotary Dar, Catherinerose Barretto, Mkurugenzi
Uendeshaji wa CCBRT, Brenda Msangi na Msanii Vanessa Mdee al-maarufu
Vee-Money ambaye pia ni Balozi wa wa Mbio za Rotary Dar kwa mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...