Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

KUFUATIA operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu ndani ya Ziwa Tanganyika inayoendelea Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga Mpina ameteketeza zana mbalimbali za uvuvi haramu zenye zaidi ya shilingi bilioni tatu zilizokuwa zikitumika katika ziwa Tanganyika.

Akiongea na wananchi baada ya zoezi la kuteketeza zana hizo haramuza uvuvi katika eneo la Businde nje kidogo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Mpina amewataka wananchi kushirikiana na serekali kwa kuwafichua wahalifu wanaotumia zana haramu ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupigwa faini na kwenda jela.

Alisema serekali haitomuonea mtu yoyote huruma ambayeatakamatwa anafanya uvuvi haramu au kuwa na zana za uvuvi haramu awe kiongozi au raia wa kawaida sheria lazima ichukue mkondo wake.''Sisi lengo letu ni kuona samaki wanaongezeka katika ziwa Tanganyika,na watu wavue kwa kufuata sheria ili Taiafa lipate mapato na watu wapate ajira"alisema

Alisema oparesheni inayofanyika katika ziwa Tanganyika ni oparesheni ya Kitaifa ya kupambana na uvuvi haramu ambayo itaendelea katika maeneo yote ya ziwa Tanganyika lengo likiwa ni kuondoa uvuvi haramu na mitandao ya wafanyabiashara wa zana haramu za kuvulia samaki wachanga na utoroshwaji wa samaki na mazao yake kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

Alisema takwimu zinaonyesha utoroshwaji wa samaki na dagaa kwenda nje katika ZIwa Tanganyika ilikuwa ni mkubwa kwenda nje ya nchi bila kulipa chochote na wageni nao kutoka nchi za jirani wanakuja kwenye maji yetu wanavua na kuondoka.
 Waziri wa Mifugo na Uvivu Luhaga Mpina akiteketeza nyavu 352 haramu za uvuvi katika eneo la Businde nje kidogo ya Manispaa ya Kigoma Ujiji zilizokamatwa kwenye oparesheni maalum ya kuzuia uvuvi haramu ndani ya ziwa Tanganyika.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiongea na wavuvi pamoja na wafanyabiashara wa mazao ya dagaa na samaki katika mwalo wa Kibirizi kabla ya kuteketeza zana haramu za Uvuvi zilizopatikana kufuatia oparesheni ya kuzuia uvuvi haramu inayoendelea katika Ziwa Tanganyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...