Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhi Mabasi 4 kwa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Jeshi la Magereza
kwaajili ya kuongezea ufanisi katika utendaji wa Kazi wa vyombo vya
ulinzi na usalama.
Mabasi 4 aliyoyakabidhi RC Makonda Leo ni Kati ya Mabasi 11 yaliyokuwa yamekufa (ukweche) ambapo baada ya RC Makonda kuyaona na kubaini uhaba wa magari kwa vyombo vya ulinzi na usalama aliwatafuta wafadhili wa Kampuni ya Dar Coach Ltd waliojitolea kuyarejeshea uhai magari hayo na hatimae leo yanatembea Barabarani yakiwa mazima.
RC Makonda amesema ukarabati wa mabasi hayo ulihusisha Kubadilisha Bodi, kupaka Rangi, kubadili Viti, kuweka Mfumo wa kuchaji simu, AC, TV, Taa,Madirisha, Matairi pamoja na kuongeza na kupunguza idadi ya viti.
Aidha RC Makonda amesema mkakati wa kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa vyombo vya ulinzi na usalama utaendelea ikiwa ni pamoja na kugusa maisha ya mtumishi mmojammoja kwa kuwapatia mikopo ya viwanja vya bei nafuu. Hata hivyo RC Makonda ameshukuru Kampuni ya Dar Coach Tanzania Ltd kwa uzalendo walioonyeaha kukarabati magari hayo pasipo kutumia pesa ya serikali.
Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi Luteni Jenerali Yacoub Mohamed amempongeza RC Makonda kwa ubunifu wa kufufua magari yaliyokuwa yamekufa ambapo ameeleza kuwa yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaongezea ufanisi katika kazi kwa kupunguza changamoto ya usafiri.
Mabasi 4 yaliyokabidhiwa leo ni Ashok Leyland 01, Iveco 2 na Toyota Coaster moja huku magari mengine 7 yakiwa hatua ya mwisho kukamilika.

wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akisalimiana na baadhi ya
Maofisa wa jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),wakati alipokwenda leo
kukabidhi Mabasi 4 kwa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Jeshi la Magereza
kwa ajili ya kuongezea ufanisi katika utendaji wa Kazi wa vyombo vya
ulinzi na usalama.
Baadhi ya magari yaliyokabidhi wa kwa JWTZ na Jeshi la Magereza
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiagana na mmoja wa Maoisa wa JWTZ,mara baada ya kukabidhi Mabasi 4 kwa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na Jeshi la Magereza
kwaajili ya kuongezea ufanisi katika utendaji wa Kazi wa vyombo vya
ulinzi na usalama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...