Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
MBUNGE wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, leo Novemba 2, 2018 amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi.
Mashtakia Zitto amesomewa mashtaka yake leo na Wakili wa serikali Mwandamizi, Tumain Kweka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi.
Wakili Kweka amedai Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya ofisi ya chama cha ACT Wazalendo mshtakiwa Zitto akiwa katika mkutano huo kwa nia ya kuleta chuki kwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la Polisi alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.
Katika shtaka la pili, kweka alidai kuwa siku na mahali hapo, Zitto akiwa Kijitonyama alitoa maneno ya uchochezi ambayo ya yalikuwa na lengo lenye kuleta hofu.Hata hivyo, mshtakiwa amekana mashtaka hayo amachiwa huru kwa dhamana na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Hata hivyo Wakili Kweka amewasilisha hati ya kiapo iliyoapwa na mkuu wa Upelelezi wa Kipolisi Mkoa wa Kinondoni SSP John Malulu ya kupinga dhamana dhidi ya Zitto.Katika hati hiyo ya kiapo wanaiomba mahakama isitoe dhamana kwa mshtakiwa kwa sababu za kiusalama, na kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, Amedai iwapo mshtakiwa huyo ataachiwa kwa dhamana ataweza kuingilia upelelezi.
Wakili Peter Kibatala anayemtetea Zitto ameiomba Mahakama impatie dhamana mteja wake na kwamba hati ya kiapo iliyowasilishwa na upande wa mashtaka mahakamani hapo inamapungufu ya kisheria ikiwamo kuwa hati ya kiapo haitakiwi kutajwa vifungu vya sheria.Kibatala alieleza kuwa hata kama kuna hati ya kiapo mahakamani, hakuna sababu za msingi zilizotolewa kuishawishi mahakama kumnyima dhamana Kabwe.
Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Shahidi amesema katika hati ya kiapo iliyowasilishwa na upande wa mashtaka ni lazima iwepo na sababu za kutosha na za msingi kupinga dhamana.Amesema ni jukumu la Polisi kulinda raia na Mali zao kwa hilo nashangaa polisi kuhofia usalama wa Zitto wakati ni jukumu lao kuhakikisha kila RAIA kuwa salama.
"Ni kweli hati ya kiapo imebeba vifungu vya sheria wakati si matakwa ya sheria kwa namna hiyo sowezi kumnyima dhamana.Hivyo Hakimu Shahidi amemtaka Zitto kuwa na mdhamini mmoja Mwenyekiti kitambulisho atakayesaini bondi ya Sh.milioni 10 Zitto amefanikiwa kutimiza masharti ya dhamana na kuachiwa huru na kesi imeahirishwa hadi Novemba 26, mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kushikiliwa katika kituo cha Polisi kwa siku kadhaa. Mh. Zitto ameachiwa kwa dhamana ya mdhamini mmoja na bondi ya sh. Milioni kumi
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, akiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa mashtaka yake yanayomkabili. Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi.
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, akiteta jambo na wakili wake Steven Mwakibolwa, kabla ya kwanza kusomewa kwa kesi hiyo katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...