Na Evaristy Masuha – Mtwara 

Serikali kupitia mradi wa uendelezaji miji Mkakati (Tanzania Strategic Cities Project) imetoa bilioni 21.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimblai ya maendeleo katika Manispaa ya Mtwara mikindani. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara 4 za mitaa kwa kiwango cha lami, Ujenzi wa maeneo matatu ya kupumzikia (Recreation Center), mfereji mkubwa wa kuondoa maji ya mvua, ujenzi wa soko la kisasa pamoja na kituo cha daladala eneo la Mikindani. 

Akizungumza leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda amesema fedha hizo zimetolewa kwa mkopo na Benki ya dunia na kwamba ujenzi wa miradi hiyo yote inatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2019. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutaufanya mji wa mtwara kuwa na muonekano mzuri na kwamba hiyo ndiyo hatua nzuri kuifanya Manispaa kuwa na sifa ya kuwa Jiji. “Naamini baada ya kukamilika miradi hii Mtwara itakuwa sehemu nyingine na pengine inaweza kupata sifa ya kuelekea kuwa jiji”. Amewataka vijana waliopata nafasi ya kuajiliwa katika ujenzi wa miundombinu hiyo kuwa waamifu ili kujijengea imani kwa waajiri. 

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa (mwenye shati Jeupe) akikagua ujenzi wa mfereji wa maji kutoka Skoya, Nabwaba, Shakuru hadi Mtepwezi.
Mfereji wa kuondoa maji kutoka Skoya, Nabwada Shakuru hadi Mtepwezi

Ujenzi wa soko la Chuno 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...