Jumuiya Kuu ya Watanzania nchini Uingereza inapenda kuwatangazia Watanzania wote na wana Africa Mashariki wanaoishi nchini Uingereza (UNITED KINGDOM) na IRELAND kuwa Sherehe za Uhuru Mwaka huu zitafanyika katika mji wa Luton siku ya Jumamosi tarehe 08/Desemba/ 2018 kuanzia saa mbili Usiku mpaka majogoo
Ifikapo saa sita usiku tutakuwa na tukio maalum litalofanywa na Mgeni rasmi pamoja wasanii maarufu wanaotegemewa kuwepo siku hiyo kukaribisha usiku wa tarehe 09/Desemba, siku ya tuliyopata Uhuru
Kutakuwa na kila aina ya vinywaji, nyama choma, chapatti’s, supu na mahanjumati ya kumwaga!
Anuani ya Ukumbi
Lewsey Farm Learning Centre Executive Hall
92 Tomlinson Avenue
Luton
LU4 0QQ
Tiketi zinapatikana kupitia akaunti maalum ya Jumuiya kwa ajili ya kuadhimisha miaka 57 ya Uhuru
Kiingilio ni £20pp, Meza moja yenye kuchukua watu nane mpaka kumi ni £200, ili kujipatia tiketi yako deposit £20 kwa mtu mmoja au £200 kwa meza kisha Tuma ujumbe kwenda anuani Pepe tzukdiaspora@gmail.com
Akaunti maalum ya Jumuiya
Jina la Akaunti- UHURU
Bank - LLOYDS
Sortcode - 30 99 08
Akaunti No. 23619960
Burudani na sound system nzito itaporomoshwa na DJ DOUBLE T, DJ CHAMBI NA DJ ANDREW
Hii si ya kukosa kwani kutakuwa na suprises za kumwaga,
UHURU DAY TUKUTANE LUTON
Imetolewa na Jumuiya Kuu ya Watanzania UK
TZUK DIASPORA
08 DECEMBER 2018.
UMOJA NI NGUVU NA PAMOJA TUNAWEZA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...