Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Taasisi ya Tiba Mifupa (MOI), Chuo Kikuu cha Yale na Emory nchini Marekani wameendesha kambi maalum ya kutoa huduma za kibingwa kupitia tiba Radiolojia ambapo wagonjwa 23 wamenufaika na tiba hiyo.

Tiba hiyo inahusisha utaalam wa kutumia vifaa vya Radiolojia kama X-Ray, MRI, CT-Scan na Ultra- Sound kutibu moja kwa moja ugonjwa au kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Radiolojia MNH, Dkt. Flora Lwakatare amesema huduma hiyo ya kibingwa ilianza kwa mara ya kwanza nchini Novemba mwaka jana ambapo kabla ya uanzishwaji wake wagonjwa waliokuwa wanahitaji huduma hizi walikuwa wakienda nje ya nchi.

Akielezea kuhusu huduma zilizitolewa katika kambi hiyo amesema ni utoaji wa sampuli kutoka kwenye vivimbe katika sehemu mbalimbali za mwili ambazo si rahisi kufikiwa bila upasuaji mkubwa, kuzibua mirija ya nyongo, kuweka mirija kwenye figo ambazo mirija ya mkojo imeziba na unyonyaji wa vivimbe vyenye maji au usaha.‘‘Kambi hii imehusisha wakufunzi ambao ni madaktari bingwa, mafundi sanifu Radiolojia, wauguzi Radiolojia kutoka vyuo vikuu vya Yale na Emory. Pia, watalaam kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa na CCBRT nao wananufaika na mafunzo hayo.’’
Mkuu wa Idara ya Radiolojia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Flora Lwakatare akizungumza na waandishi wa habari juu ya wataalam kuzibua njia ya nyongo ya mgonjwa kupitia huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Chuo Kikuu cha Yale na Emory nchini Marekani. Kutoka Kushoto ni daktari bingwa wa upasuaji wa Muhimbili, Dkt Godfrey Mchele na mtaalam wa tiba ya radiolojia, Profesa Frank Minja kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani.
Baadhi ya wataalam wa tiba hiyo pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Dkt. Flora Lwakatare.
Wataalam wa radiolojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) pamoja na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Yale na Emory nchini Marekani wakishirikiana kuzibua njia ya nyongo ya mgonjwa kupitia huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia.
Mtaalam wa tiba radiolojia, Profesa Frank Minja kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu jinsi wataalam wa Muhimbili, MUHAS na MOI walivyofanya maandalizi ya kufanikisha huduma ya tiba radiolojia. Kushoto ni Dkt. Lwakatare na kulia ni mtaalam wa huduma za radiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Emory nchini Marekani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...