
Akizungumza katika mahojiano maalum amesema kuwa miradi hiyo itajikita katika sekta za Kilimo, Ufugaji, Elimu, Afya ambapo itawawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi na kujiletea maendeleo .
“ Tumelenga kujenga Mabwawa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa Wilaya yetu ina ardhi yenye rutuba na wananchi wanao uwezo mkubwa wa kushiriki katika uzalishaji kupitia sekta hii ndio maana tumeamua kuweka mikakati ya kukuza uzalishaji na kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda”. Alisisitiza Mhe. Msuya
Akifafanua amesema kuwa kilimo cha umwagiliaji kitasaidia kuongeza uzalishaji wa mpunga pamoja na mazao mengine ya biashara yatakayochochea ustawi wa wananchi na kukuza uchumi kwa ujumla.
Akizungumzia huduma za afya amesema kuwa Wilaya hiyo imepokea shilingi Bilioni moja na nusu kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo na tayari maandalizi ya ujenzi yameanza ambapo mradi huo utakapokamilika utakuwa ukombozi mkubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo na maeneo ya jirani.
Alitaja miradi mingine inayotekelezwa katika Wilaya hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha Afya katika jimbo la Igalula kilichogharimu milioni 400 ambapo ujenzi wake uko katika hatua za mwisho kukamilika ili wananchi waanze kupata huduma.
Kwa upande wa kituo cha Afya Utege kilichopo jimbo la Tabora Kaskazini Mhe. Msuya amebainisha kuwa kimekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo hali inayoonesha dhamira safi ya Serikali kuleta ustawi kwa wananchi kwa kuboresha huduma za afya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...