*Ahimiza ushiriki wao kwenye ujenzi wa viwanda
*Aahidi kutoa milioni 700/- Chuo cha Polisi Dar


Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ametoa maagizo kwa vyombo vya ulinzi na salama kujipanga kwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za uchumi ikiwemo ujenzi wa viwanda nchini.

Ametoa kauli hiyo leo Desemba 21, 2018 jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mafunzo ya maofisa wa Polisi na wakaguzi wasaidizi wa jeshi hilo zilizofanyika viwanja vya Chuo cha Polisi ambapo amesisiiza umuhimu wa vyombo vya ulinzi kujikita kwenye shughuli za kiuchumi.

"Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama jipangeni kushiriki kwenye kujenga uchumi wa nchi yetu.Hakuna ubaya kuwa na kiwanda cha kutengeneza viatu, maji na nafaka.Sioni sababu ya kila mara jeshi la polisi kupewa mchele kutoka kwa watu binafsi.Jeshi la Magereza mnao wafungwa ambao wanapaswa kulima na kuzalisha chakula cha kutosha ambacho mnaweza kukigawa kwa taasisi nyingine,"amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo Rais Dk.Magufuli ameahidi kutoa Sh.milioni 700 kwa lengo la kuboresha Chuo cha Polisi jijini Dar es Salaam na kutaka fedha hizo zitumike vizuri na kinyume na hapo zitageuka kuwa kaa la moto huku akisistiza ameamua kutoa fedha hizo kwa lengo la kulinda heshima na hadhi ya chuo hicho.

"Fedha hizo nitazitoa kabla ya Ijumaa ya wiki ijayo , kubwa zaidi fedha hizo zitumike kwa malengo ambayo nimeyakusudia.Nimekusikia Mkuu wa Chuo hichi cha Polisi Naibu Kamishna wa Polisi (DCP)Anthony Rutta ukiomba Sh.milioni 700 nitakuletea ili parekebishwe na kupendeza .Najua sisi Serikali tunahamia Dodoma lakini hapa chuoni lazima pawe pazuri na pakuvutia.

"Kwa Jeshi la Magereza niliamua kutoa fedha ili kujengwe nyumba z askari lakini hazikujengwa , wakati mwingine unapata shida kwasababu unatoa fedha zijengwe nyumba lakini hazijengwi.Nimeshatoa maagizo hizo fedha zifuatiliwe ili nijue zilikopotelea,"amesema Rais Magufuli.
 Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia Viongozi wa Majeshi na Serikali pamoja na Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika hafla ya kufunga Mafunzo ambapo jumla Askari 513 wakiwemo Maafisa wa Polisi 120 na Wakaguzi Wasaidizi 393 wamehitimu katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Jijini Dar es salaam.Desemba 21,2018 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...