Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


JUKWAA la Lishe Tanzania (PANITA) limesema kuna mambo kadhaa mazuri ambayo yamefanywa kwa mwaka huu 2018 katika eneo linalohusu lishe nchini Tanzania huku likitoa ushauri kwa Serikali kuhakikisha eneo la lishe linapewa kipaumbele zaidi kwa mwaka ujao wa 2019.

PANITA limetoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam baada ya Michuzi Blog kutaka kufahamu ni mambo gani mazuri ambayo yamefanyika katika eneo la lishe kwa mwaka huu 2018 ambao umebakisha siku moja ya kesho kumalizika.

Uongozi wa PANITA pamoja na mambo mengine mazuri ambayo yamefanywa na wadau wa masuala ya lishe nchini, umesema kwa mwaka huu 2018 wamefurahishwa na ongezeko la bajeti iliyotengwa kwa ajili ya lishe toka Sh.bilioni 11 kwa mwaka 2017/18 mpaka Sh.bilioni 14 mwaka 2018/19.Pia wamezungumzia kufurahishwa na kusainiwa kwa mikataba ya kutekeleza afua za lishe kati ya wakuu wa mikoa na Makamu wa Rais kupitia Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imeongeza uwajibikaji wa Lishe katika ngazi zote.

"Tukiri kwa mwaka huu kuna mambo mengi mazuri ambayo yamefanyika na kuonesha jitihada za dhati katika kuhakikisha eneo la lishe kwa Watanzania lipata nafasi ya kuwepewa kipaumbele.Kumewepo na mikutano ya mipango na bajeti za lishe iliyoshirikisha pia asasi imeongeza umiliki wa mipango.Pia Ofisi ya Waziri Mkuu kuahidi kutunga sheria ya kubana,"amesema.

Uongozi wa PANITA umefafanua Waziri mkuu aliahidi kushawishi Bunge kuwe na sheria ya kubana fedha za lishe zisitumike vinginevyo.PANITA imetoa mwito umefika wakati kuwa na vyanzo vya fedha vya ndani katika 
kushughulikia suala la lishe ili kupunguza utegemezi wa wafadhili

.Pia wameshauri Serikali kujenga nyumba za kunyonyeshea ili kuwapa nafasi ya kunyonyesha watoto vizuri hususani miji yenye foleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...