Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kusimamia miradi ya maji kwa umakini mkubwa.
Amewataka DAWASA kuhakikisha kufikia 2020 asilimia 85 ya vijijini na asilimia 95 ya mijini inapata maji safi na salama. Mkumbo amesema hayo wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya jengo la Maji lililopo Ubungo jijini Dar es Salaama na linalotarajiwa kumalizaika Februari 2020.
Utiaji wa saini hiyo ulihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja. Akizungumza baada ya utiaji wa saini, Mkumbo amesema DAWASA lazima wahakikishe wanasimamia mapato ili kuweza kuendeleza miradi ya maji ili wananchi waweze kufaidika.
Amesema, hafla ya leo sio ya kukabidhiwa jengo tu ila wanatakiwa kusimamia mradi wa Kidunda, visima vya Kimbiji Mpera pamoja na kuwaunganishia wateja wapya. Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi Mwamunyage amesema changamoto kubwa iliyokuwepo katika mamlaka hiyo ni maeneo ya kufanyia kazi ila baada ya kukabidhiwa jengo hilo wanaamini kwa sasa kazi zitafanyika kwa wakati.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo akizungumza na
wanahabari na wageni waalikwa wakati wa utilianaji wa saini wa
usimamizi wa jengo la Maji lililokuwa likijengwa na Wizara ya maji na
Umwagiliaji na sasa wamekabidhiwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa ajili ya kulimalizia na kuhamishia ofisi. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyage akizungumza na wanahabari na wageni waalikwa
wakati wa utilianaji wa saini wa usimamizi wa jengo la Maji lililokuwa
likijengwa na Wizara ya maji na Umwagiliaji na sasa wamekabidhiwa DAWASA
kwa ajili ya kulimalizia na kuhamishia ofisi. Kulia ni Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo na kushoto ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa machache.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (kushoto) akisaini mkataba na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (katikati) wa
kusimimia jengo la Maji House linalotarajiwa kumalizika Februari 2020.
Pambeni kulia ni mmoja ya wajenzi wa kampuni ya CCECC ambao ndiyo
wakandarasi. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...