MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Mwanasha Tumbo amesema atashirikiana na wanamichezo ili kuhakikisha wanaweza mazingira mazuri yatakayowezesha kupatikana timu ambayo itaweza kushiriki ligi madaraja ya juu ikiwemo Ligi kuu.

Mwanasha aliyasema hayo wakati fainali michuano ya kombe la Kabunda Cup iliyokuwa ikichezwa kwenye viwanja vya Vikonge Mtindiro wilayani Muheza ambapo alisema ili kuweza kuhakikisha wanafanikisha jambo hilo wataendelea kuhamasisha vijana kujikita kwenye michezo.

Alisema licha ya kuhamasisha michezo kutokana na kwamba ni ajira ambayo inaweza kuwainua vijana kuichumi na kupata maendeleo lakini pia aliwahaidi kuwajengea kiwanja cha mpira chenye matofali ili waweze kuonyesha umahiri wao na hatimaye wilaya hiyo iweze kupata mafanikio kwenye soka.

“Leo nimekuja hapa kuhimitisha Ligi hii kwanza nimefurahishwa sana na viwango ambavyo mmekuwa mkivionyesha kwenye mchezo huu nimeongeza na Diwani wenu hapa na niwahaidi kwamba nitawajengea kiwanja chenye matofali ili hari ya kushiriki kwenye michezo muweza kuendelea nayo na tunaamini siku zijazo tutairudisha Muheza kwenye ramani ya soka “Alisema DC Mwanasha.

MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati akifunga Mashindano ya Kombe la Kabunda Cup

MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Mashindano ya Kabunda Cup Nahodha wa timu ya Ushirika Amiri Nko kushoto ni Afisa Michezo wa wilaya ya Muheza Anania Sama
Nahodha wa timu ya Ushirika Amiri Nkoa akiwa ameinua kombe hilo juu mara baada ya kukabidhiwa 
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akimkabidhi Kitita cha Milioni moja Nahodha wa timu ya Ushirika Amiri Nko baada ya timu yao kuibuka na ushindi kwenye michuano ya Kombe la Kabunda Cup kushoto ni Afisa Michezo wa wilaya ya Muheza Anania Sama .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...