Mkurugenzi Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Albert Richard amemweleza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye kuwa UCSAF imeleta changamoto chanya kwa kampuni za simu za mkononi zinazotoa huduma za mawasiliano nchini.

Richard ameyasema hayo wakati wa ziara ya Nditiye ya kukagua changamoto za mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali wilayani Sengerema mkoani Mwanza.  Richard amefafanua kuwa awali kampuni za simu za mkononi nchini zilisita kuwekeza kwenye vijiji mbali mbali ambavyo havina mawasiliano nchini kwa kuwa havina mvuto wa kibiashara ambapo kampuni hizo zilikuwa zinakwenda maeneo ya mijini yenye mvuto wa kibiashara.

“Ila sasa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano tunashirikiana na kampuni za simu za mkononi kufikisha huduma za mawasiliano vijijini na kampuni zimepata mwako,” amesema Richard. Ameongeza kuwa Serikali imekuwa inatoa ruzuku kwa kampuni hizo ili waweze kujenga minara kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za mawasiliano.

Nditiye amesema kuwa amefanya ziara ya siku tatu ya kukagua mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali wilayani Sengerema ili kuona changamoto za mawasiliano ambapo amekiri uwepo wa changamoto za mawasiliano kwenye Wilaya hiyo kwenye baadhi ya kata ambapo ina jumla ya kata 21 na kubaini uwepo wa ukosefu wa mawasiliano kabisa kwenye baadhi ya maeneo, mawasiliano ya kusuasua na mahitaji ya kuongeza nguvu ya usikivu wa mawasiliano kwenye baadhi ya maeneo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia) akisikiliza kwa makini taarifa kutoka kwa Afisa Mtendaji Kata ya Katwe, Wilaya ya Sengerema, Mwanza, Deus Ngodagula Masasi (aliyenyoosha kidole) kuhusu ukosefu wa mawasiliano kwenye kisiwa cha Maisome wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya mawasiliano wilayani humo. Naibu Katibu Mkuu – Sekta ya Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi (aliyeshika ramani) akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji, UCSAF, Mhandisi Albert Richard (wa kwanza kushoto).
Naibu Katibu Mkuu – Wizara Ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi (aliyeinua mkono) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua changamoto ya mawasiliano kisiwani Maisome, Mwanza. Anayesikiliza wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Dkt. Jones Kilimbe.
Diwani wa Kata ya Bangwe, wilayani Sengerema, Mwanza, Yonas Magikulu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya mawasiliano Wilayani humo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara Ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...