Na Felix Mwagara, MOHA-Bukoba.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Askari Polisi nchini kukamata pikipiki wakiwa hawana sare za Jeshi.
Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa uhuru, Mayunga, mjini Bukoba Mkoani Kagera, leo, Lugola alisema polisi wanapaswa kufuata utaratibu wa kijeshi hasa wanapokamata vyombo vya moto na siyo kuvunja utaratibu.
Lugola aliongeza kuwa, bodaboda zinazovunja sheria za usalama barabarani zinapaswa kukamatwa bila kuwaonea huruma, ila ni kosa Polisi kuwanyanyasa vijana hao ambao wanapata ridhiki kupitia biasahara hiyo. “Mnapaswa kukamata hizi bodaboda zinapofanya makosa, tabia ya kukurupuka huku mkitafuta fedha zisizo halali, huko ni kuwaonea waendesha bodaboda,” alisema Lugola.
Pia Lugola aliwataka waendesha bodaboda mjini Bukoba na Tanzania kwa ujumla wafuate sharia za usalama barabarani zikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa. Lugola ameanza ziara yake ya siku nane mkoani humo akitembelea Wilaya zote za Mkoa huo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na mamia ya
wananchi mjini Bukoba Mkoani Kagera, katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Mayunga mjini humo, leo. Lugola licha ya
kuwa amewataka waendesha bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani,
lakini ametoa onyo kwa Polisi mjini humo kuacha kuwakamata waendesha
bodaboda wakiwa hawajavaa sare.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsikiliza Mkazi wa
mjini Bukoba alipokuwa anaeleza kero yake mara baada ya Waziri huyo
kuwaita wananchi hao mbele waweze kutoa kero zao, mara baada ya kumaliza
kuzungumza na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika
Uwanja wa Uhuru, Mayunga mjini humo, leo. Lugola licha ya kuwa amewataka
waendesha bodaboda wafuate sheria za usalama barabarani, lakini ametoa
onyo kwa Polisi mjini humo kuacha kuwakamata waendesha bodaboda wakiwa
hawajavaa sare.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimsalimia Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Bashiru Ally, wakati alipoonana
naye Uwanja wa Ndege wa Bukoba, leo. Lugola yupo Mkoani Kagera kwa ziara
ya kikazi akitembelea Wilaya zote, akisikiliza kero mbalimbali za
watumishi wa Wizara yake pamoja na wananchi mkoani humo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akitoka Kituo Kikuu
cha Polisi cha mjini Bukoba mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza
katika Kituo hicho, leo, kwa kufuatilia utendaji kazi wao. Katikati ni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, na kulia ni Mkuu wa
Jeshi la Magereza Mkoani humo, ACP Raymond Mwampashe. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...