NA DENIS MLOWE, IRINGA

MWENYEKITI wa Serikali za vyuo vikuu vya Kikatoriki chini, Anord Mvamba ametoa wito kwa vijana kujenga utamaduni wa kutembelea vituo vinavyowalea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu sanjari na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo hatua itakayowasaidia kufikia malengo yao.

Ametoa rai hiyo juzi mara baada ya kujumuika pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Tosamaganga kilichoko wilaya ya Iringa mkoani Iringa wakati akiadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.

Mvamba alisema kuwa kundi la watu wasiojiweza wanahitaji kupata misaada kutoka kwa jamii inayowazunguka na hasa vijana ambao wamekuwa wakitumia sehemu ya fedha katika mambo ya starehe zaidi kuliko kuwajali yatima ili wapate furaha.

Aliongeza kuwa ni vema kuona umuhimu na haja ya kuwasaidia ili wapate faraja hivyo na katika kusherehekea kumbukizi ya kuzaliwa kwake ameona umuhimu kama kijana kutoa sadaka na kusheherekea na watoto ho kwa wa vitu mbalimbali vikiwemo, chumvi, sukari, sabuni na vifaa vya shule.

Mvamba ambaye pia ni rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Ruaha Iringa (RUCU)alisema kuwa endapo vijana wengi wakijenga tabia ya kuwatembelea watoto yatima na wanaoshi katika mazingira magumu itakuwa fursa kwao kujifunza zaidi na kuwa na moyo wa huruma katika kuwasaidia kuliko kupoteza fedha nyingi katika starehe ambazo ni za muda mfupi tofauti na kuwekeza katika watu.

Aidha ameitaka jamii kujitolea kwa dhati kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji, ikiwa pamoja na kuwatembelea ili kujenga upendo kwa makundi maalumu yenye uhitaji kwa lengo la kupunguza changamoto zinazoyakabili makundi hayo.

Kwa upande wake,Sister Helena Kihwele ni msimamizi mkuu wa kituo cha watoto Yatima cha Tosamaganga alisema kituo kina jumla ya watoto 60 ambao hawajafikisha mwezi mmoja hadi miaka sita, na kuwa changamoto kubwa ni walezi kuwasahau watoto mara baada ya kukabidhiwa kituoni hapo.

“Changamoto hii inatusumbua sana maana baadhi ya walezi hawaji kuwasalimia wala kuwachukua watoto sasa tunapata shida wakati wanapotakiwa kurudi nyumbani, maana umri wa mwisho wa kukaa kituoni hapa ni miaka 6,” alisema Kihwele

Alisema kituo kinapokea watoto wasio na mama au wenye mama ambaye ni anatatizo la akili, na kuwa baadhi ya ndugu ndiyo wamekuwa wakiwatelekeza watoto mara tu wanapowafikisha kituoni hapo.

Changamoto nyingine zinazowakabili watoto ni baadhi ya wazazi kushindwa kuwaendeleza kielimu watoto, kwani baadhi ya walezi huwa hawana mwamko wa kuwaendeleza watoto hao, na hivyo kusababisha watoto hao kutoendelea na masomo.
Mwenyekiti wa Serikali za vyuo vikuu vya Kikatoliki chini, Anord Mvamba ambaye pia ni Rais wa Serikalia ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Ruaha Iringa, (RUCU) akimkabidhi moja vitu mbalimbali mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Tosamaganga kilichoko wilaya ya Iringa mkoani Iringa Helena Kihwele wakati akiadhimisha siku ya kuzaliwa mwanzoni mwa ka. (picha na Denis Mlowe)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...