Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
MWANAMUZIKI nchini ya Nigeria David Adeleke, maarufu kama Davido amechaguliwa kushiriki kwa mara nyingine katika Tuzo za kimataifa za Nickelodeon kwa mwaka huu.
Miongoni mwa wanamuziki wanaoshindanishwa na Davido katika tuzo hiyo kwenye kipengele cha Mwanamuziki anaependwa wa kimataifa ni pamoja na Taylor Swift, David Guetta na J Balvin kutoka amerika ya kusini
Davido akiwa msanii mwenye umri wa miaka 26 kwa mwaka huu imekua fursa kwake kwa mara ya pili kushiriki katika tuzo hizo kutoka Afrika huku akishindanishwa na wasanii kutoka mataifa mbalimbali.
Na usiku wa Tuzo hizo utapambwa Na Msanii djKhaleed ambae kwa msimu uliopita alijizolea tuzo tatu ikiwemo tuzo ya rapa bora wa mwaka pamoja na Msanii bora wa mwaka kimataifa huku wimbo wa No brainer aliomshirikisha Msanii Justin Bieber kuibuka wimbo bora wa mwaka.
Pia wasanii ambao wamebahatika kuwepo kwenye vipengele tofauti tofauti katika tuzo ni Cardi B, Ariana Grande, Maroon 5, Camila Cabello ambao wanafanya vizuri kwa sasa kimataifa kwenye soko la muziki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...