Mwanariadha Makoye Bundala (501) wa Shinyanga akimaliza mbio za mita 100 wavulana mbele ya Mwanariadha aliyeshika nafasi ya pili Matiko Nyamalaga (289) wa Mara na mwanariadha Steven Stephano wa Tabora (601) wakati wa hatua ya fainali zilizofanyika leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu mtwara. 
Wanariadha kutoka kundi la wasichana Shija Donald wa Mwanza (387) akiwaongoza wakimbiaji wenzake kumaliza fainali za mbio za mita 100 leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara 
Baadhi ya wakimbiaji wa mbio za mita 400 x4 wakijiandaa kwa ajili ya mchuano wa nusu fainali wa mbio hizo zilizofanyika leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara 
……………………….. 

Na Mathew Kwembe, Mtwara 

Mwanariadha wa Shinyanga Makoye Bundala ameibuka kuwa mshindi wa kwanza katika fainali za mbio za mita 100 za mashindano ya UMITASHUMTA zilizofanyika leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara. 

Makoye alitumia muda wa sekunde 11:87, ambapo aliyemfuatia ni Matiko Nyamalaga kutoka mkoani Mara ambaye alitumia muda wa sekunde 11:94, na nafasi ya tatu ilichukuliwa na mwanariadha Steven Stephano wa Tabora ambaye alitumia muda wa sekunde 12:07 kumaliza mbio hizo. 

Kwa wasichana, mshindi wa fainali za mbio za mita 100 ni Shija Donald wa Mwanza ambaye alitumia muda wa sekunde 13:16 kumaliza mbio hizo, nafasi ya pili ilichukuliwa na Paulina Pius pia wa Mwanza ambaye alitumia muda wa sekunde 13:38, huku nafasi ya tatu ilichukuliwa na Fauzia Hamu wa Singida ambaye alitumia muda wa sekunde 13:91. 

Katika mchezo wa kurusha mkuki nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mwanafunzi Suzan Wilson wa Mbeya ambaye alirusha mkuki umbali wa mita 33 na sentimita 94, nafasi ya pili ilichukuliwa na Vatheline Amri wa Tabora ambaye alirusha mkuki umbali wa mita 31 na sentimita 80, huku nafasi ya tatu ilichukuliwa na Paskalina Augustino wa Manyara aliyetumia umbali wa mita 29 na sentimita 40.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...