Na Khadija seif,Globu ya jamii
MASHINDANO ya miss kinondoni yazinduliwa rasmi jijini Dar es salaam
Mratibu wa mashindano hayo Nancy kikwembe ( super model) amesema mashindano hayo yamefunguliwa rasmi na kufanikiwa kupata warembo takribani 18.
"Mchakato ulianza muda mrefu taingia mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu na matangazo yalikua mengi na warembo 46 walijitokeza ,"
Super model amesema katika mchuano huo wanategemea kupata mrembo atakaewakilisha vizuri katika wilaya ya kinondoni na kufanikiwa kuingia miss Tanzania.
"Julai 13 mashindano ya kumpata miss kinondoni yatafanyika katika ukumbi wa life park jijini Dar es salaam,"
Hata hivyo mratibu huyo amesema zawadi kwa mshindi wa Kwanza atapatiwa gari aina ya Min Cooper yenye thamani ya shilingi milioni 13,huku mshindi wa pili atapata seti ya vitu vya ndani ikiwemo kitanda,godoro pamoja na viti.
"Mshindi wa tatu atapatiwa televisheni pamoja na king'amuzi huku mshindi wa nne na watano watapatiwa vifuta jasho,"
Aidha,amewaomba wadhamini wajitokeze ili kufanikisha shindano hilo kwani mabalozi mbalimbali hutokea kwenye mashindano ya mamiss kutokana na mionekano yao pamoja na akili na nidhamu.
Mratibu wa mashindano ya miss kinondoni Nancy Joseph (super model) akizungumza na waandishi wahabari wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo life park jijini Dar es salaam.
Gari aina ya Min copper ambayo itatolewa kwa mshindi wa Kwanza wa miss kinondoni mwaka huu jijini Dar es salaam.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...