
Mkurugenzi wa Ansaf bw. Audax Rukonge, akiwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya kisera kutoka kwa wanachama na wadau mbalimbali kutoka taasisi binafsi zinazoshughulika na maendeleo ya sekta ya kilimo nchini

Mkurugenzi wa Ansaf bw. Audax Rukonge, akiwasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya kisera mbele ya waandishi wa habari morogoro
Jukwaa huru la wadau wa kilimo nchini(ANSAF) limewasilisha mapendekezo ya mabadiliko ya kisera kutoka kwa wanachama na wadau mbalimbali kutoka taasisi binafsi zinazoshughulika na maendeleo ya sekta ya kilimo nchini. Zoezi la uwasilishaji wa mapendekezo ya mabadiliko ya sera ya kilimo nchini lilitangazwa na Wizara ya kilimo kupitia tangazo la Katibu mkuu Mhandisi Mathew John Mtigumwe tarehe 04.06.2019
Akiwasilisha mapendekezo hayo katika mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Ansaf bw. Audax Rukonge ameipongeza serikali ya awamu ya 5 kupitia wizara ya kilimo kuweza kushirikisha wadau katika utoaji wa maoni kwa lengo la kuboresha sera ya taifa ya kilimo ya mwaka 2013.
“sera ya kilimo inatambua umuhimu wa miundombinu katika maendeleo ya kilimo na ili kukuza kilimo kunahitajika kuwekeza kwenye miundombinu ya nishati, umwagiliaji, usafirishaji wa mazao kutoka vijijini masoko na uhifadhi wa mazao” alisema bw. Rukonge
Baada ya hapo bw. Rukonge aliwasilisha mapendekezo yafuatayo:


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...