Na Said Mwishehe, Michuzi TV

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dk.Josephat Gwajima ametinga Ikulu ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza wazi kwamba ili ule Chips Mayai ni lazima baadhi ya mayai yavunjike.

Ameeleza namna ambavyo anafurahishwa na jitihada za Rais Dk.John Magufuli za kuleta maendeleo huku akitumia nafasi hiyo kumshukuru kwa jitihada zake za ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika Bonde la Mto Rufuji maarufu kwa jina la Stiegler.

Akizungumza leo Juni 3,2019 akiwa Ikulu jijini Dar es Salaam, Askofu Dk.Gwajima amesema ni jambo nzuri kutoa shukrani kwa Rais Dk.John Magufuli kwa jitihada zake za kuleta maendeleo na hasa katika kuimarisha sekta ya nishati ya umeme.

"Kwanza ni jambo nzuri kuelewa ili ule Chips Mayai lazima uvunje baadhi mayai. Kuna mayai lazima yavunje.Namshukuru Rais kwa juhudi zake katika mradi wa umeme wa Stiegler, mahala ambapo tutazalisha umeme mwingi tofauti na hapo zamani .

"Kumbuka wakati wa Mwalim Nyerere,wakati wa Mwinyi, wakati wa Mkapa na wakati wa Jakaya Kikwete tulikuwa tunazalisha umeme kiasi lakini kupitia .... tutazalisha umeme mwingi kuliko Tanzania ilipoanzia,"amesema Askofu Gwajima.

Ameongeza kama ambavyo inafahamika watu wengi wa nchi za Magharibi wanasema eneo hilo ni kwa ajili ya mazingira pamoja na mambo mengine lakini ukweli hizo ni siasa za kimataifa.

"Kwa mfano ukiangalia miaka iliyopita kulikuwa na mkataba kule Japani uliokuwa unafahamika Mkataba wa Kioto na Marekani walikataa kusaini ule mkataba.Hivyo hata sisi tunatakiwa kulinda Interest zetu,"amesema Askofu Gwajima.

Kuhusu ujumbe wake kwa Watanzania,Askofu Gwajima amesema huu ni wakati wa kukimbia na si kutembea hivyo lazima twende na kasi ya dunia."Dunia inakimbia hivyo lazima nasi Watanzania tukimbie ili twende pamoja na dunia."
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Naibu Waziri Ofisi wa Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira Anthony Mavunde wakwanza kutoka kushoto. PICHA NA IKULU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...