Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau wa mazingira wakiwemo FORUMCC wamezindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Mazingira.

Wakati wa uzinduzi huo viongozi wa Halmashauri hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wamehimiza wananchi wote kuendelea kuuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuhakikisha mazingira yanakuwa safi wakati wote.

Akizungumza kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mjema amesema kuna kila sababu kila mmoja wetu kuungana na Serikali katika kukomesha matumizi ya mifuko ya Plastiki na kufafanua katika wiki hii ya mazingira kutafanyika kampeni ya nguvu ya kuhamasisha utunzaji mazingira.

"Ilala tumejipanga na tutaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha usafi wa mazingira inaendelea kuwa kipaumbele chetu.Tukatae mifuko ya Plastiki,tukae uchafu,"amesema Mjema.

Kwa upende wake Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Rebecca Muna amesema kupitia Mradi wa Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya(EU) wataendelea kushirikiana na Ilala na Serikali kwa ujumla kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na changamoto za kimazingira

"Hii ni wiki ya mazingira,hivyo sisi FORUMCC chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya tumekuwa na mradi wa mabadiliko ya tabianchi na mazingira.Tumekuwa tukifanya kazi na Serikali na kwa Dar es Salaam tunashirikiana na Ilala na kwa kweli zinakwenda vizuri.

"FORUMCC tunaridhishwa na namna ambavyo viongozi wa Serikali ya Tanzania ambavyo nimejipanga na wako mstari wa mbele katika suala la mazingira na Tabianchi.Tunafahamu Serikali imepiga marufuku mifuko ya plastiki,nasi ni wajibu wetu kuunga mkono,"amesema.

Awali wakati anamkaribisha Mkuu wa Wilaya kuzungumza na wadau wa mazingira,Kaimu Meya wa Ilala Omar Kumbilamoto ametumia nafasi hiyo kueleza wanatambua mchango wa wadau hao kwani wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha Ilala inakuwa safi.

Hata hivyo amesema kupitia kikao kilichoitishwa na FORUMCC kwa kushirikiana na Ilala kuna mambo kadhaa ambayo yamejitokeza kwa upende wa wakandarasi wa kuzoa taka ,hivyo watakutana nao kujadiliana kwa kina na hatimaye kuondoa changamoto zilizoko.

"Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,mazingira safi katika wilaya yetu ni kutokana na wadau wa mazingira tulionao ambao wanafanya kazi kubwa sana.Hata hivyo kilio chao ni muda uliowekwa kwenye mkataba wa uzoaji taka.Wamewekewa mwaka mmoja mmoja wakati zamani ilikuwa miaka mitatu,tutakaa tuone tunafanyaje,"amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Sophia Mjema akiwa amebeba kikapu ikiwa ni ishara kwa wananchi kutumia mfuko mbadala baada ya kuanza kutekelezwa kwa sheria ambayo imezuia matumizi ya mifuko ya plastiki.Mjema alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira inayoanza leo na kumaliza Juni 5,mwaka huu
Kaimu Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Omari Kumbilamoto (aliyesimama)akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema(wa kwanza kulia)akiwa anasikiliza jambo kwa umakini wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mazingira.Wengine walioko waliokuwa naye ni viongozi wa Wilaya ya Ilala
Viongozi wa Wilaya ya Ilala wakiwa pamoja na wadau wa mazingira wakiwa wenye picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mkuu wa FORUMCC Rebecca Muna(wa kwanza kushoto)akiwa na mwanamuziki wa Singeli Msaga Sumu wakipata burudani.
Wadau wa mazingira wakiburudika kwa nyimbo za Singeli wakati Mwanamuziki Msaga Sumu akitumbuiza.
Wasanii wa FORUMCC wakitoa  burudani kwa wadau wa mazingira

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...