Wananchi wa Kata sita zilizokumbwa na mafuriko Wilayani Kyela, wameiomba serikali kuwatafutia maeneo mapya ya makazi.
Wamesema, kutokana na Kata hizo kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hasa nyakati za misimu ya mvua, wameona kuna haja ya wao kuondoka na kwenda kuishi kwenye maeneo ya miinuko.
Ombi hilo, wamelitoa leo wakati wakizungumza na mwandishi wa Michuzi Blog, alipotembelea eneo hilo na kushuhudia uharibifu wa mali za watu na mazingira uliosababishwa na mafuriko hayo.Baadhi ya Kata zilizokumbwa na mafuriko hayo ni Kata ya Ikama, Kajunjumale, Katumbasomgwe na Talatala.
Akizungumzia hilo, baadhi ya watu waliokumbwa na kadhia hiyo, Elia Mwakipesile na Kasutu Mwambandile, wamesema hali ilivyo sasa wapo tayari kuyahama maeneo hayo ya mabondeni lakini wanaiomba serikali kuwatafutia maeneo mengine rafiki.
Hata hivyo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, imetembelea eneo hilo na kutoa pole ya shilingi miloni moja na kusisitiza kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuachana na tabia ya kujenga mabondeni.
"Suala la kuhamisha watu waliojenga mabondeni halijawahi kuwa jambo rahisi sana, mtakumbuka majanga yaliyotokea jangwani ilibidi hadi nyumba zivunjwe kwahiyo hata huku lazima elimu itolowe, ” amesema.
Jumla ya watu sita wanasadikiwa kupoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za April 29 na Mei 11 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya (Kulia) Mh Albert Chalamila akimkabidhi Fedha kiasi cha Shilingi Mil 1 ili Mkuu wa Wilaya ya Kyela Cloudia Kitta ili kusaidia katika uboreshaji wa Miundombinu ya barabara ambayo imeathirika na Mafuriko

Eneo la Mashamba ya Mapunga kijjiji Cha Bujonde Kata Kajunjumele ambayo yaliathiriwa kwa kiasi kikubwa na mafuriko yaliyotokana na Mvua zilizotokea April 29 na Mei 11 Mwaka huu.

Mzee Elia Mwakipesile Mkazi wa Kijiji cha Bujonde Wilaya ya Kyela ambaye ni mmoja wa waathirika wa mafuriko yaliyotokea April 29 na Mei 11 Mwaka na Kusababisha Vifo vya watu 6
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...