Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

VYOMBO vya dola Mkoani Kigoma vimefanikiwa kumkamata kijana Hussein Hamis maarufu(Orosho)anayetuhumiwa kuwa kinara wa ubakaji na kujeruhi wanawake kinguvu kingono nyakati za usiku.

Kijana huyo aliyekamatwa pamoja na watuhumiwa wengine tisa wakitambuliwa kama"teleza"ambapo huwaingia kingono akina wanawake kinguvu,kuwaibia na kuwajeruhi wakiwa wanejipaka oil chafu au mafuta ya mawese ili wanaposhika wawe wanateleza.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Kigoma mjini Samson Hanga amesema kuwa baada ya kuwepo taarifa hiyo ya vijana wanaoingilia akina mama kingono kwa nguvu vyombo vya dola viliendesha zoezi la msako mkali kwa kushirikiana na wananchi ili kuweza kuwakamata wahalifu.

"Tulitengeneza namna namna bora ya kuwakamata wahusika ambapo tulifanya zoezi la upigaji kura ya siri tukapata majina na majina mengine tulipata kupitia vyombo vya dola mpaka sasa tumesha kamata vijana 9 wapo mahabusu na upelelezi unaendelea"alisema

Hanga alisema kuwa katika majina yaliyotajwa na kupigiwa kura mtuhumiwa mmoja alitajwa sana na akina mama waliofanyiwa vitendo vya ukatili ambaye ni Hussein Hamis(Orosho).

"Unajua serikali ina mkono mrefu na macho makubwa yule kijana alipopataarifa kuwa tunamtafuta alikimbilia kwa mama yake kijiji cha Kagongo baadae akakimbia tena kijiji cha Kagunga juzi jioni tukafanikiwa kumkamata Wilayani Kasulu na kuletwa hapa kituo cha polisi kwaajili ya hatua zaidi"alisema

Alisema pia wamefanya gwaride la utambuzi kwa wahanga kuwatambua hao vijana 10 waliokamatwa.Alisema msako bado unaendelea yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja kabla vyombo vya dola havijambaini na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote watakaobainika.

Hadija Khamis Mkazi wa mwanga kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji ni mmoja wahanga wa matukio ya "teleza"ameishukuru serikali kwa kufanikiwa kuwakamata vijana waliokuwa wanafanya vitendo vya kikatili kwa wanawake hasa wa kata za mwanga kusini na kaskazini.

"Unajua hadi sasa yaani siamini kama kweli "teleza amekamatwa tulikuwa tunaishi bila ya amani mimi alipoingia kwangu alinikata na panga mara nne hapa nina maumivu makali hata kazi siwezi kufanya"alisema

"Hawa wapo wengi mimi sababu matukio yanaweza tokea usiku mmoja hata mawili kwa maeneo tofauti serikali iwachukulie hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine na tabia hii iweze kuisha kabisa"alisema

Martha Jerome Mkurugenzi wa asasi ya women promotion Center amesema suala la "teleza"linaumiza mioyo wanaiomba serikali kusaidiana na jamii kutokomeza swala hili.

"Unajua sasa hivi suala la "teleza"limekuwa gumzo Kigoma kwakweli linaumiza moyo,kinatuumiza sisi kama asasi tutahakikisha tunashirikiana na serikali kutokomeza suala hili tutaingia mtaani,naiomba serikali,viongozi wa dini asasi mbalimbali tusaidiane kutokomeza hili jambo"alisema
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Hanga akitoa taarifa kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu kukamatwa kwa vijana 10 wanaotuhumiwa kwa matukio ya kuwaingilia kinguvu wanawake na kuwaibia pamoja na kuwajeruhi maarufu kwa jina la "teleza"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...