Madaktari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wakimsikiliza Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Khuzeima Khunbhai kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiwaeleza jinsi wagonjwa waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (CCU) wanavyotibiwa. Madaktari hao walifanya ziara ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu wanazozitoa.
Madaktari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wakimsikiliza Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi Delila Kimambo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiwaeleza jinsi duka la dawa la Taasisi hiyo linavyotoa huduma kwa wagonjwa. Madaktari hao walifanya ziara ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu wanazozitoa.
Dk. Adarsh Tiwathia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) akiongea jambo wakati wa kikao na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yao ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu wanazozitoa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na madaktari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wakati wa ziara yao ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo na mishipa ya damu wanazozitoa.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...