Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo ametembelea eneo la Mathias Kata ya Miyuji Jijini Dodoma kujionea adha na changamoto ya kivuko wanayopata wananchi wa eneo hilo kutokana na uwepo wa korongo kubwa ambalo hupitisha maji mengi kipindi cha mvua na hivyo kukatisha mawasiliano kati ya eneo hilo na maeneo mengine.
Akiongea kwa niaba ya wananchi wa eneo hilo,Diwani wa Kata ya Miyuji Mh David Mgongo ameeleza changamoto hiyo kubwa kiasi cha kupelekea wanafunzi kushindwa kwenda Shule kipindi cha Mvua na wananchi kukosa huduma muhimu kutokana na adha hiyo.
Mbunge Mavunde amewahakikishia wananchi hao kujengwa kwa kivuko hicho ndani ya muda mfupi kama ambavyo aliahidi wakati wa Kampeni na kwamba mkandarasi amepatikana na fedha kiasi cha Tsh 199,000,000 zitatumika kwa ajili ya ujenzi huo chini ya TARURA na shughuli rasmi za Ujenzi zitaanza wiki ya Tarehe 3.06.2019 ,pia Mbunge Mavunde ameahidi kujenga kivuko kidogo cha watembea kwa miguu ambacho kitajegwa mita 70 kutoka kivuko kikubwa kinapojengwa.
Wananchi wa eneo hilo wamemshukuru sana Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele kushughulikia matatizo yao na kuahidi kujitolea nguvukazi wakati wa zoezi lote la ujenzi ili na wao kuunga mkono juhudi za Mbunge huyo.
Sehemu ya kivuko chenye changamoto kwa wakazi wa kijiji cha Mathias.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu wa Bunge,Kazi,Ajira na Watu wenye Ulamavu Anthony Mavunde akitoa maelekezo kuhisiana na suluhisho ya kivuko katika eneo la Mathias wakati alipofanya ziara hapo.
Naibu Waziri Anthony Mavunde akipita katika kivuko hicho
Naibu Waziri nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu wa Bunge, Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Anthony Mavunde akiangalia Kivuko katika eneo la Mathias Kata ya Miyuji kilicho haribika kutokana na mvua za hivi karibuni.
Naibu Waziri Anthony Mavunde akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mathias kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili Wananchi wa kijiji hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...