Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WANAFUNZI 100 kutoka Shule za Serikali na binafsi wamechaguliwa kujiunga kwenye timu ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano ya UMISETA ambayo yanatarajiwa kufanyika mkoani Mtwara.

Waliochaguliwa kujiunga na timu ya Mkoa wa Dar es Salaam ni baada ya kufanyika kwa mashindano ya UMISETA kwa ngazi ya Wilaya ambapo zote zilishiriki na kupitia mashindano wamepatikana wanafunzi hao ambao wapo wa michezo mbalimbali.

Akizungumza baada ya kutajwa majina ya wanafunzi hao kati ya wanafunzi 500 walioshiriki ngazi ya Wilaya ,Katibu Tawala Msaidizi(Utawala na Utumishi)Mkoa wa Dar es Salaam Lawrence Malangwa

amewataka wanafunzi wote kuwa na nidhamu kwa kipindi chote watakachokuwa kwenye mashindano hayo huku akionya ni marufuku kutumia mamluki kwani vijana hao wanasifa zote zinazostahili.

Amesema anaamini walimu waliochaguliwa kwenda na wanafunzi hao watakuwa makini kuhakikisha wenye sifa wanapata nafasi ya kushiriki mashindano hayo na wanauhakika Mkoa wa Dar es Salaam wataibuka washindi wa jumla

Pia ameagiza wanafunzi waliochaguliwa kwa ngazi ya Mkoa kwenda kwenye mashindano hayo kabla ya kuondoka wapimwe afya zao ili kuwa na uhakika wa uimara wa afya kabla hawajaondoka.

Malamgwa ameongeza wanafunzi hao wanatakiwa kutambua wakati wanajiandaa kwenda Mtwara watambue wamepewa dhamana ya kuwawakilisha wanafunzi wote wa sekondari kwa Mkoa wa Dar es Salaam na hivyo wanapaswa kujituma na kuonesha bidii wakiwa mchezoni

Kwa upande wake Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam Hamis Lissu amesema kuwa wamejiandaa vizuri na watarudi na ushindi mnono wa kitaifa na kwamba wao wanakwenda kutetea ubingwa wao kwani miaka yote wamekuwa wataibuka washindi katika mashindano hayo.

Lissu amefafanua wanafunzi hao wanatoka katika shule za serikali na binafsi na waliochaguliwa wamepatikana baada ya kufanyika kwa mashindano kwa wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam.

Amefafanua wakati wa wote wa mashindano kwa ngazi ya Wilaya hakuna mwanafunzi yoyote ambaye ameumia na hilo ni jambo la kujipongeza.
Walimu na mwanafunzi kutoka Wilaya ya Ilala wakikabidhiwa Kombe baada ya kuibuka washindi wa jumla katika mashindano ya UMISETA ngazi ya Wilaya

Mmoja wa wanafunzi wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam akipokea kikombe kutoka kwa mgeni rasmi kabla ya kutangazwa kwa.majina ya wanafunzi waliochaguliwa kwa ngazi ya Mkoa kwa ajili ya mashindano hayo
 Wanafunzi wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakishangilia baada ya kuibuka washindi wa jumla  kwenye mashindano ya UMISETA kwa ngazi ya Wilaya
 Baadhi ya wanafunzi ambao wamechaguliwa kuuwakilisha Mkoa wa Dar es Salaam kwenye mashindano ya UMISETA wakipatiwa utararibu na maelezo kuhusu mashindano hayo
Walimu kutoka shule za sekondari Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kichaguliwa kuungana na  wanafunzi 100 kutoka Mkoa huo wanaokwenda kushiriki mashindano ya UMISETA yanayotarajia kufanyika mkoani Mtwara 
Wanafunzi  wa shule za sekondari Wilaya ya Ilala Dar es Salaam wameibuka washindi wa pili kwa ngazi ya Wilaya katika mashindano ya UMISETA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...