Na Humphrey Sha, Globu ya Jamii Nkasi.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesikia kilio cha muda mrefu cha watumiaji wa bandari ndogo ya Kabwe iliyopo wilayani Nkasi mkoani Rukwa, kwa kuanza ujenzi wa bandari kubwa ya kisasa itakayomaliza changamoto zilizopo hivi sasa.

Bandari ya sasa ya Kabwe iliyopo katika mwambao wa Ziwa Tanganyika ina gati dogo ambalo limelalamikiwa na wasafirishaji kuwa wakati wa kiangazi maji yanapungua hadi kufikia kina cha mita moja na hivyo kulazimika kupakia mizigo ndani ya maji kwa kutumia boti ndogo.

Akizungumza na waandishi wa habari bandarini hapo Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese, amesema Bandari ya Kabwe ni kitovu cha biashara kati ya mkoa wa Rukwa na mikoa mingine na kati ya Tanzania na nchi jirani hivyo ina umuhimu mkubwa kwa ustawi wa uchumi.

Amesema kutokana na umuhimu huo sambamba na changamoto za bandari ndogo ya sasa Serikali kupitia TPA ilitoa fedha Sh bilioni 7.49 kwaajili ya ujenzi wa bandari mpya ya kisasa itakayoendana na mahitaji ya sasa na ya baadae.

Amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 74 kuingia majini, ujenzi wa jengo la abiria, ghala, nyumba za watumishi, jengo la mgahawa na uzio utakaozunguka eneo lote la bandari.

Ametaja kuwa mradi huo unaotekelezwa na Mkandarasi M/S Sumry's Enterprises Ltd ulianza Aprili Mosi 2018 na unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 24 sawa na miaka miwili na kwamba hadi sasa umefikia asilimia 40.

Meneja huyo amesema mradi huo ukikamilika utaongeza ufanisi wa huduma za bandari hiyo na kuingiza mapato zaidi.

Kwa mujibu wa Afisa Bandari ya Kabwe, Mohamed Mahyoro bandari hiyo licha ya changamoto zilizopo meli na shehena zimekuwa zikiongekeza mwaka hadi mwaka na kwamba hiyo ni ishara kwamba kuna biashara kubwa katika bandari hiyo.

"Kuanzia Julai 2017 hadi Juni 2018 tulihudumia tani 14,550 na kuanzia Julai 2018 hadi Mei mwaka huu bandari hiyo ndogo imehudumia tani 19, 591 na kwa upande wa maboti yaliyohudumiwa katika kipindi cha Julai 2017 hadi Juni 2018 yalikua 259 na Julai 2018 hadi Mei mwaka huu imeshahudumia meli 319," alisema Mahyoro.

Mahyoro alisema changamoto iliyopo ni kina cha maji kupungua hadi mita moja na wakati wa mvua huongezeka na kifikia mita 1.5.Mfanyabiashara Mohamed Shabib ambaye anatumia bandari hiyo kusafirisha mizigo yake alisema ujio wa bandari mpya utamaliza changamoto ya ufupi wa kina cha maji.

"Hapa kuna shida ya kina cha maji na tunalazimika kujaza mzigo kwenye maboti makubwa ndani ya maji kwa kutumia boti ndogo hivyo tunashkuru mradi huu mpya utatuondolea kero hii ambayo inaongeza gharama," alisema Shabib.
 Meneja Bandari za Ziwa Tanganyika Ajuaye Msese akizungumza na Waandishi wa Habari waliofika katika bandari ya Kabwe Mkoani Rukwa Wilaya ya Nkasi kujionea shughuliA ujenzi wa gati mpya inavyoendelea.
 Moja ya Mafundi wa Gati ya Bandari ya Kabwe Ziwa Tanganyika akiwa ameibuka kutoka kwenye maji ambapo anazamia kwa ajili ya kupanga mawe.
 Mafundi was kufuma nguzo zinazo zamishwa kwenye maji wakiendelea na shughuli yao katika mradi huo unaogharimu zaidi ya Bilioni 7.
 Afisa Bandari ya Kabwe Mohamed Mahyoro akizungumza na Waandishi wa Habari
Sehemu ya majahazi yanayopakilia mzigo ndani ya Maji kwa sasa kutokana na changamoto ya kutokuwey kwa gati yenue kina kizuti na Cha kutosha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...