*Yajikita katika kuwanoa vijana zaidi ili waweze kujiajiri wenyewe kupitia viwanda

Na Leandra Gabriel, Michuzi Tv
KATIKA kuadhimisha maonesho  ya 43 ya biashara maarufu Kama sabasaba Mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA)wamejizatiti katika kuendana na kasi ya awamu ya tano ambayo kwa kiasi kikubwa imejikita zaidi katika kujenga uchumi wa viwanda na kulipeleka taifa katika uchumi wa Kati.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Michuzi Tv mara baada ya kuwatembelea katika banda lao la maonesho katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, wadau mbalimbali wameeleza namna VETA inavyoshiriki kwa kiasi kikubwa katika kuchangia ukuaji wa kiuchumi hasa kwa kuzalisha vijana waliobobea katika fani mbalimbali.

Akieleza namna wanavyoshiriki katika shughuli za kilimo Gema Ngoo ambaye ni mkufunzi wa masomo ya kilimo amesema kuwa wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali juu ya kilimo bora na cha kisasa zaidi ili kuweza kuzalisha mazao yanayoendana na soko kwa Sasa.

"Maarifa mengi yanatolewa kwa vijana na sio katika kilimo pekee pia na namna ya kupambana na wanyama waharibifu, hapa tuna ndege aina ya tai ambaye  ametengenezwa kitaalamu na anaweza kutembea takribani katika hekta kumi kufukuza wanyama waharibifu, pia tuna mafunzo ya umeme, upishi, useremala na vingine vingi" ameeleza Ngoo.

Aidha amesema kuwa VETA wataendelea kushirikiana na serikali na taasisi nyingine ili kuhakikisha azma ya serikali ya awamu ya tano inafikiwa na amewataka vijana kutembelea katika banda lao ili waweze kupata ujuzi wa namna ya kujiajiri wenyewe.

Vilevile William Mnuo ambaye ni mkufunzi wa magari hasa magari makubwa yakiwemo mabasi ameeleza kuwa wapo makini katika kuhakikisha wataalamu hasa madereva wanaozalishwa kutoka VETA wanakuwa wa mfano na mabalozi bora kwa wenzao.

Mnuo amesema kuwa maarifa na ustadi unaotolewa na VETA kote nchini umelenga katika kuwakomboa vijana kutoka katika  mawazo ya kuajiriwa na kuweza kujiajiri wenyewe.
 William Mnuo ambaye ni mkufunzi wa magari makubwa kutoka VETA akizungumza na Michuzi Tv ambapo amesema kuwa wataendelea kutoa mafunzo wa vijana ili kuzidi kuzalisha vijana waliobobea katika fani mbalimbali zinazotolewa na vyuo hivyo vya ufundi, leo jijini Dar es Salaam.
 Gema Ngoo mkufunzi wa masuala ya kilimo akizungumza na Michuzi Tv na kueleza kuwa vijana wasitegee zaidi katika kujiajiri kwani mafunzo yanayotolewa na VETA ni mtaji tosha wa kuweza kujiajiri, leo jijini Dar es Salaam.
 Rose Mushi mwanafunzi wa VETA mwaka wa pili akitoa maelekezo ya namna mashine ya kuoka nyama waliyoibuni inavyofanya kazi, leo jijini Dar Es Salaam.
Sussack Mbulu mwalimu wa VETA kutoka Mkoa wa Ruvuma akitoa maelekezo ya namna mashine ya kubangulia kwa wakulima wadogo aliyoibuni inavyofanya kazi, leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...