JOSEPH MPANGALA , MTWARA.
“Walimuita Mke wangu nikamwambia Uende lakini mke wangu akaogopa akaenda akiwa amembeba mwanangu mmoja wa kike wakamshika kwa nguvu na kuondoka naye na mimi wakaniambia Niondoke”anasema Ahmad Msham Kijana anayejishughulisha na kilimo cha Mahindi,Mpunga na Kunde katika kijiji cha Mtole Kilichopo Nchini Msumbiji Mpakani mwa Tanzania.
Ahmad Msham Mtanzania alikuwa akiishi kijiji cha Mtole anasema Juni26 Usiku wa kuamkia alhamis Baadhia ya watu waliovalia Mavazi ya Jeshi la Msumbiji walivamia Kijiji cha Mtole kilichopo Msumbiji na kuanza kuchoma moto nyumba na baadae kuwakusanya wananchii pamoja na kuanza kuwaua kwa kuwapiga risasi ,tisa wakiwa Watanzania na wawili Raia wa msumbiji
Mke wake Halima Hassan Lyanga pamoja na mmoja wa Mtoto wake Zarahna mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu alichukuliwa na Watu hao huku yeye akiachiwa mtoto wa kiume Zahran ambao ni mapacha mpaka sasa Hawajulikani walipo.
Msham ameiomba serikali kusaidi ili kuwezesha kupatikana kwa Mke na mtoto ambao mpaka sasa hakuna taari zozote zinazoonesha kuwa wamepelekwa wapi.
Aidha Diwani wa Kata ya KitayaJamal Kapende amesema kuwa baadhi ya wakazi wa kata yake wanashiriki shughuli za kilimo katika Kijiji cha Mtole kilichopo mpakani mwa Tanzania kwa makubaliano na serikali ya Vijiji pamoja wanakijiji Husika kutokana na kuwapo na maeneo mazuri kwa kilimo.
Kapende anasema Katika watu Tisa waliokufa ni wanakijiji Saba wanatoka Kijiji cha Kitaya na hivyo kuleta majonzi kutokana na kfahamika na wanakijiji hao.
“Sisi Tumepatwa na simanzi kubwa isitoshe kuna Watanzania watatu ambao hawajulikani kama wakufa au wapo Salama,kuna mama ambaye alikuwa na watoto mapacha wamemchukua yeye na mtoto mmoja wakamuacha mtoto mmoja na Mumewe wake na Kuna Binti amechukuliwa jambo ambalo wakazi wa kata hii wamekuwa na Huzuni Kubwa”amesema Kapende ambaye ni Diwani wa Kata ya Kitaya.
Hata Hivyo Mkuu wa jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka wakazi wa Kata Hiyo Kuhakikisha wanaonesha ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ili kuweza kufanikisha Upatikanaji wa wananchii waliochukuliwa pamoja na Uwapo na Amani katika eneo hilo la mpakani.
“Tunadhamana kubwa ya Kuwalinda nyinyi na yoote yanawezekana tukishirikiana, sikuzote tunasema Taarifa ndio kitu cha msingi wewe ukimuona mtoto wako tatizo unamashaka naye tuambie,ukimuona mumeo tatizo unamashaka naye tuambie,ukiona mpenzi wako tatizo tuambie kwasababu usipofanya hivyo hata msikitini utashindwa kwenda hata makanisani utashindwa kwenda”IGP Sirro.
Jumapili ya wiki hii IGP Simon Sirro anatarajia kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi kutoka Nchini Msumbiji ili kutatua tatizo hilo lililopo Mpakani.
Ahmad Msham akiwa amembeba Mtoto wake Zahran huku akimsikiliza Inspekta jenerali wa polisi IGP Simon Sirro wakati akiongea na wananchii wa kata ya Kitaya katika uwanja wa Mahakamani Mtwara Vijijini.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akiongea na wanannchii wa kijiji cha Kitaya Mkoani Mtwara Juu ya utoaji wa Taarifa kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa lengo la kuimarisha Ulinzi na Usalama.
Ahmad Msham akiongea mbele ya IGP Simon Sirro kuhusiana na kuchukuliwa kwa Mke pamoja na mtoto wake katika kijiji cha Mtole kilichopo Msumbiji mpakani mwa Tanzania ambapo mpaka sasa hawajulikani walipo.
Baadhi ya wananchiii wa kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara wakimsikiliza IGP Saimon Sirro katika mkutano baada ya kutokea mauaji ya Watanzania Tisa katika Kijiji cha Kitole kilichopo Msumbiji Mpakani mwa Tanzania.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...