Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
KAMISHNA Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi wa Taifa wa Ziwa Manyara Noel Myonga amesema mwitikio wa Watanzania kutembelea hifadhi za Taifa ni mdogo, hivyo ameshauri kuongeza kasi ya kutembelea vivutio vilivyopo nchini.
Akizungumza leo Juni 28,2019 na waandishi wa habari waliofanya ziara wakiwa na walimbwende wa taji la Mrembo wa Mkoa wa Arusha waliotembelea hifadhi hiyo Myonga amesema ni vema Watanzania wakajenga utamaduni wa kutemebela hifadhi zilizopo nchini.
"Kutembelea hifadhi zetu kunasaidia mambo mengi sana ikiwemo kujifunza jografia ya nchi yetu, kuona vivutio vilivyopo na hatimaye kuongeza pato la nchi pamoja a kujiburudisha kwani kuna kila kitu ambacho mhusika anataka kukiona kama sehemu ya kupata starehe,"amesema Myonga.
Amevitaja baadhi ya vivutio vinavyopatikana kwenye hifadhi ya Manyara ni pamoja na kuona Simba wapandao juu ya miti, Ziwa Manyara pamoja na chemchem ya maji moto.
Amesema wamekuwa wakiwahamasisha Watanzania wanaotutembelea hifadhi hiyo na kuwashawishi kwenda kwa wingi na kwamba katika kufanikisha hilo wamekuwa wakijitagaza mara nyigi lakini mwitikio ni mdogo.
Aidha amesema sio kwamba Watanzania hawana uwezo, bali utamaduni au mwamko wa kuwekeza fedha kwa ajili ya kutembelea kama wageni wa nje bado hawaoni thamani ya kufanya hivi, tukiamua tunaweza.
"Mtanzania anaona ni bora aende bar akatumie fedha kuliko kuja hifadhini ,ila naomba wabadilike kwa kuamua kutembelea hifadhi zetu badala ya kwenda kwenye maeneo mengine peke yake.Ukija hapa unalipa Sh.11,800 za kiingilio pamoja na VAT), gharama za usafiri ni kidogo kwa Mtanzania,"amesema Myonga.
Kwa upande wake Mhifadhi Ujirani mwema Ibrahimu Ninga ametumia nafasi hiyo kuzungumzia tatizo la ujangili katika hifadhi hiyo ambapo amesema moja ya jambo ambalo liliwahi kumnyima usingizi, ni matukio ya ujangili ambao kwa kweli yalisababisha wanyama kama vile tembo kuuawa kwa wingi
"Kazi ya kupambana na ujangili ni ngumu, lakini wao tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa, ndio maana mapaka sasa hali imetulia.Majangiri wana wanakuwa na mbinu nyingi kila kukicha, nasi tumejizitati kwelikweli, tumeimarisha doria zetu, tunashirikiana na wananchi ambao wanazunguka hifadhi hii na vyombo vingine vya dola kupambana na tatizo hili,"amesema Ninga.
Ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kufanya kazi kubwa na wamekuwa hawalali ili kupambana na tatizo hilo."Nakumbuka ilifikia hatua majangili yalianza kutumia sumu kuua wanyama kwa wanyama ambao wanakula maboga kama tembo, wengi walikufa."
kamishina msaidizi mwandamizi wa uhifadhi wa Taifa wa ziwa Manyara Noela Myonga akielezea historia ya ziwa manyara
muhifadhi ujirani mwema Ibrahimu Ninga akiongoza watalii wa ndani kwenda kuona chem chem ya maji moto iliopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara
Wageni kutoka nchi ya Uingereza waliotembelea hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara wakiwa katika moja ya kuvutio kili chopo ndani ya hifadhi hii wakiwa wanagusa maji ya chem chem ya maji moto kuhakikisha kama kweli kama maji haya ni yamoto






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...