Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dkt Mshindo Msolla amesema kuwa katika kilele cha siku ya mwananchi kutakuwa na matukio matatu muhimu.

Kilele cha siku ya mwananchi kinatarajiwa kuwa Julai 27 mwaka huu tutakuwa na matukio matatu ambapo kwanza kutambulisha jezi mpya za msimu wa 2019/20, pili ni utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliosalia na tatu ni mchezo kimataifa wa kirafiki. 

Dkt Msolla amesema, katika kuelekea kilele cha siku ya mwananchi kutatanguliwa na shughuli mbalimbali za kijamii ndani ya wiki nzima ikiwemo kufanya usafi kwenye mahospitali.

Akizungumzia usajili wa msimu mpya na ripoti ya kocha mkuu Mwinyi Zahera, Dkt Msolla amesema wamesajili kulingana na matakwa ya mwalimu, pamoja na ukocha wake kwa miaka 40 wamesimamja uweledi na kufuata kile kocha alichokiandika kwenye ripoti yake.

"Naamini hata huko alipo lazima atakuwa anafuraha maana wachezaji wote wa nje na ndani aliokuwa akiwahitaji tumewapata pia siku tatu zilizopita mwalimu alituma program ya mazoezi ,sisi kama menejimenti tumejipanga kuhakikisha yote yanaenda sawa" amesema Dkt Msolla.

"Kwa wale wachezaji wote ambao hawatakuwa nao msimu ujao kila mmoja ameshapewa barua ya kujulishwa suala hilo na si jambo jema wachezaji hao kuwatangaza hadharani kwani huenda baadhi yao wakapokea taarifa hiyo kwa namna nyingine," amesema.

Mbali na hilo, uongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wake Dkt Msolla umetoa onyo na kutangaza rasmi kutokufumbia macho watengenezaji wa jezi feki wanaotumia nembo ya Klabu yao.

Amesema, amewapa siku nne wale wote wanaotumia nembo ya klabu kwa ajili ya utengenezaji wa jezi na vifaa mbalimbali kwa manufaa yao ya kibiashara na baada ya tarehe 30 mwezi huu mtu yeyote atakaejihusisha na uuzaji wa jezi feki hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yake.

Mwenyekiti amesema kuwa lengo ni kuwaita wafanyabiashara hao wa uuzaji wa jezi na kufanya nao mazungumzo kujua ni namna gani wanaweza kusaidiana kwenye swala hilo la mauzo ya jezi na vifaa mbalimbali vyenye nembo ya klabu.
Mwenyekiti wa Yanga Dkt Mshindo Msolla(kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kilele cha siku ya mwananchi Julai 27 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...