KAMPUNI WAASILI ASILIA YAHAMIZA WATANZANIA KUCHANGAMKIA BIDHAA ZA NGOZI ZINAZOZALISHWA NCHINI
Na Mwandishi Wetu, Blog ya Jamii
WATANZANIA wameshauriwa kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini ili kuchochea wazawa kufanya vizuri zaidi kwenye soko la ndani na nje ya nchi.
Mwito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Kampuni ya waasili asilia Limited ambayo inatengeneza bidhaa za ngozi asilia ya Tanzania Dedan Munis katika viwanja vya maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa.
Amesema pamekuwepo na kasumba mbaya kwa watanzania kupenda bidhaa za kigeni badala ya kupenda zinazozalishwa na watanzania wezao ambao pia wanatengeneza ajira kwa vijana wa kitanzania.
Amesema iko shida kubwa kwa watanzania kwani wanapenda sana bidhaa za nje kuliko za ndani jambo ambalo linazolotesha bidhaa za ndani ukizingatia kuwa bidhaa hizi zinatengenezwa katika kiwango cha juu na cha ubora tena kwa Mali ghafi za ndani.
"Ndugu waandishi kimsingi nawakaribisha wananchi watanzania wezangu hapa sabasaba katika majengo haya ya Jakaya Kikwete Banda na 31,32waje wapate bidhaa bora zaidi zinazotengezwa na watanzania wenyewe kupitia Kampuni ya waasili asilia limited." Alisema Munisi.
Nakuongeza kuwa hapo kuna changamoto ya uwepo wa bidhaa Kutoka nje ambazo pia ni za plastiki na Mara zote watanzania ndio wanakimbilia,lakini nivema wananchi wakafika katika Banda hilo la Jakaya kikwete ili kujionea vitu vizuri vinavyozalishwa na wazawa katika kiwango cha ubora.
Amesema mwaka huu wamejipanga zaidi kushinda mwakajana kwani wanabidhaa bora zaidi kama vile viatu vya ngozi aina zote,sandles kwa akina mama na akina Baba na hata watoto mabegi kwa (handbegi) na vitu vingine vingi na tena vinapatikana kwa gharama nafuu.
Amesema katika kumuunga mkono Rais katika azima yake ya viwanda basi wao wamefanya kwa vitendo na ameweza kuajiri watanzania wakutosha tu japo bado changamoto mbalimbali zipo ila wanapambana nazo.
"kama watanzania kwa sehemu yetu tumeamua kuweka kikubwa Serikali iendelee kuruboreshea Mazingira ya kufanya biashara pamoja na kuruhu taasisi za Fedha kutoa mikopo pasipo kuwa na riba kubwa," amesema Munisi.
Amefafanua watanzania wakumbuke kuwa wakipenda bidhaa za ndani kimsingi zinaleta na kuhifadhi utamaduni halisi wa mtanzania na mwaafrika kwa ujumla hivyo wananchi wajitokeze kwenye Banda hilo la Jakaya Kikwete.

Mkurugenzi wa Kampuni ya wa asili asilia Dedan Munisi alifafanua jambo kwenye maonyesho ya 43 ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Wilayani Temeke leo.picha na Mpiga picha wetu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...