Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
*Amuagiza Katibu Mkuu (Sekta ya Ujenzi) kupatiwa majina ya Wasimamizi wa miradi hiyo.
*Ujenzi wa Mradi Nyumba za Magomeni Kota, wakamilika kwa asilimia 40
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) kupatiwa majina ya Wasimamizi wa Miradi mbalimbali nchini inayosimamiwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA) kuangalia Taaluma zao.
Waziri Kamwelwe ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari alipotembelea mradi wa ujenzi wa Nyumba maarufu Magomeni Kota unaoendelea jijini Dar es Salaam.Amesema Serikali imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 2 kukamilika mradi huo, amesema kinachoonekana katika ujenzi wa nyumba hizo hakiridhishi.
"Nimebaini hakuona watu wanaofanya kazi, ujenzi umelala na sio kwa sababu ya fedha, kwani htiwezi kuingia mikataba halafu baadae tunawalipa?" amehoji Waziri Kamwelwe."Fedha ya Serikali haiwezi kufanya mafunzo kwa Wataalamu, sasa naagiza Miradi yote ya nchi nzima wale Wasimamizi wenye Taaluma nipate majina yao nataka kila mradi uwe na msimamizi wake", amesema Waziri Kamwelwe.
Hata hivyo, Waziri Kamwelwe amefanya ziara katika mradi wa nyumba uliopo Bunju B jijini Da es Salaam, ambapo amesifu ubora wa nyumba hizo zilizojengwa kwa viwango vinavyokubalika.Amesema amepeleka mapendekezo kwa Serikali Kuu kuhusu nyumba ambazo zimenunuliwa na Watumishi wa Serikali na tayari Watumishi hao wamehamia makao makuu Dodoma, amependekeza kwa Serikali kwa Watumishi hao kubadilishiwa nyumba hizo zilizopo Dar es Salaam na zile za Dodoma.
Mradi wa ujenzi wa Bunju B jijini Dar es Salaam una viwanja 851 kwa ajili ya makazi ya Watumishi na ujenzi huo unatekelezwa kulingana na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (aliyevaa suti nyeusi) akipata maelekezo kutoka kwa Mmoja wa Wataalamu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) kwenye mradi wa Nyumba za Makazi uliopo Magomeni Kota.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akipata maelekezo ya sehemu ya ndani katika ujenzi wa Nyumba za Magomeni Kota.
Majengo yanayoendelea kujengwa katika eneo la Magomeni Kota.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akiwa ameongozana na Wataalamu wa TBA katika mradi wa ujenzi wa Nyumba za Bunju B jijini Dar es Salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...