Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Kufuatia hali ya Udumavu na Lishe duni kwa asilimia Kubwa ya Watoto katika Kaya nyingi zinazopatika Mkoani Kagera, Imeonekana kuwa Suluhisho pekee la kuondokana na changamoto hiyo ni Kutumia chakula dawa, chenye virutubishi maalum kwa ajili ya Afya ya Mtoto.

Shirika la Kimataifa linalohusiana na masuala ya Afya na Lishe Bora, lijulikanalo kama IMA World Health Tawi la Mkoa wa Kagera, kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara yenye dhamana, linaendelea na Kampeni yake Mkoani humo iitwayo "Mtoto Mwelevu, Ni Jukumu langu" lengo likiwa ni kuhakikisha tatizo la Udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika Mikoa ya kanda ya ziwa, Kagera ikiwa ni mmojawapo linapungua kwa asilimia kubwa.

Akizungumza Katika Tamasha la Mtoto Mwelevu Katika Kata ya Buyango Wilayani Missenyi, Juni 27, 2019. Afisa Afya Mkoa wa Kagera Nelson Lumberi kwa Niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa, amesema Jamii ina wajibu mkubwa katika kuzingatia suala la Lishe bora kwa watoto, ikiwa tunalenga kupunguza Udumavu Mkoani Kagera, na Lishe hiyo ni vyakula vya kawaida ambavyo upatikanaji wake ni rahisi kwani hupatikana zaidi katika mazingira yao, hivyo suala linabaki namna ya kupangilia mlo na hatimae kupatikana kwa matokeo Bora ya Mtoto anayekua, na Mtoto mwenye akili.

Tayari IMA World Health wamekwishaanza utaratibu huo kwa kuziendea Kaya ambazo suala la lishe limekuwa changamoto katika Halmshauri za Mkoa wa Kagera, Missenyi, ikiwa mojawapo kwa kutoa mafunzo ya Lishe kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo, Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii (WAJA) Ambapo Jamii inaelekezwa namna ya kuandaa Chakula Dawa, ambapo katika Kata ya Buyango watoto waliofanyiwa tathimini na Mradi kwa kupimwa kiwango cha utapiamlo Jumla ni 541, kati ya hao waliogundulika na utapiamlo ni 114 ambapo waliingizwa kwenye Darasa la Chakula Dawa kwa Siku 12. 

Kati ya hao watoto 6 hawakuhudhuria na mmoja wapo kupoteza Maisha na kufanya idadi kuwa watoto 107 walioendelea na Kumaliza Darasa. Siku ya 12 asilimia 83 ya watoto waliongezeka uzito na asilimia 55 Afya zao ziliimarika. Wazazi mpaka sasa wanaendelea na zoezi hilo nyumbani ambapo Afya za watoto 107 zimeendelea kuimarika.

Hayo yanajiri ambapo Takwimu zikionesha kuwa hali ya Udumavu Nchini ni asilimia 34.7 wakati Mkoa wa Kagera Udumavu ni asilimia 41.7 hivyo Shirika la IMA World Health wakijitahidi kupunguza kiwango hicho kwa asilimia 7 kufifikia 2020.


Pichani ni Bi. Geniva Ereneus (30) Mama Wa watoto Mapacha Oliva na Olivia Ereneus akiendelea kuwalisha Chakula Dawa katika Tamasha la Mtoto Mwelevu Kata Buyango, Wilaya ya Missenyi.
Mtoto Safina Ahmad (4) akiendelea kunywa uji Wa lishe ambao ni Chakula dawa, wakati wa Tamasha la Mtoto Mwelevu Wilayani Missenyi kama alivyokutwa kamera yetu.
Pichani ni Afisa Afya Mkoa wa Kagera Nelson Lumberi akizungumza na wananchi waliohudhuria Tamasha la Mtoto Mwelevu, kwa niaba ya Mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa Kagera.
Pichani ni Wadau kutoka IMA World Health na wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii (WAJA) wakifurahia Tamasha la Mtoto Mwelevu kwa kucheza ngoma ya asili, katika hafla iliyofanyika Wilayani Missenyi.
Pichani ni Sehemu ya Wazazi na walezi kutoka Kata Buyango, wakiwa katika Tamasha la Mtoto Mwelevu lililofanyika Katika Zahanati ya Kata Buyango, Wilayani Missenyi Juni 27, 2019.
Pichani ni mmoja kati ya akina mama waliohudhuria Tamasha la Mtoto Mwelevu, baada ya kumgawia mwanae Chakula Dawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...