Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyopewa mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji imemuhukumu kifungo cha miaka miwili gerezani Mhandisi wa kampuni ya Best World Engineering, Novat Kaberwa, baada ya kukiri kumuua mke wake, Clara Munisi bila kukusudia.
Kaberwa anadaiwa kumpiga mke wake, baada ya kurudi nyumbani saa tatu usiku na kukuta watoto wameshinda njaa na mama yao (marehemu) kutokujulikana alipokwenda, huku akirudi akiwa amelewa kwa kutumia hela ya matumizi aliyoacha mume wake nyumbani.
Hukumu hiyo imesomwa leo Julai 24, na Msajili, Pamela Mazengo, baada ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali, Justus Ndibalema na kukubali kuwa ni kweli alimuua mke wake bila kukusudia.
Kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo, msajili Mazengo amesema, amezingatia hoja zilizotolewa na mawakili wa utetezi kuwa mshtakiwa ameweza kuipunguzia gharama ma usumbufu Mahakama kwa kukiri kosa na pia amezingatia mazingira ya tukio yalivyotokea, hivyo mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka miwili jela.
Mapema, Wakili wa utetezi, Venance Victor akishirikiana na Hashimu Mziray na Neema Kalabuha, waliiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wao kwa sababu hilo ndiyo kosa lake la kwanza na pia ana watoto wawili ambao hawana mtu wa kuwaangalia.
Victor amedai mteja wao amekaa mahabusu tangu Julai 15, 2016, na kwa kipindi chote hicho, cha zaidi ya miaka mitatu amejifunza na amebadilika, ambapo hadi sasa hakuna kosa lolote alilolitenda akiwa gerezani na amebadilika na pia anajutia alichokitenda.
Aidha, wakili huyo aliiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wake huyo kwani amesomeshwa na Serikali mchepuo ya sayansi na bado serikali inamuhitaji aweze kukamilisha miradi ambayo alipewa na serikali.

" Kumbukumbu zinaonesha mshtakiwa pamoja na kampuni yake ya Best World Engineering ilikuwa imepewa mradi wa kurekebisha barabara ya Mikumi na Kilosa, hadi sasa Serikali imeshindwa kutekeleza kwa wakati kwa sababu mshtakiwa yupo ndani,"amedai Victor.
Wakili huyo, katika kumtetea mshtakiwa aliongeza kudai kuwa, katika tukio hilo hakuna silaha yoyote iliyotumika kuonesha alifanya kitendo hicho kwa kudhamilia na pia ukizingatia marehemu hakufia eneo la tukio, alifia hospitali.
Naye wakili, Neema aliiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wao huyo kwani watoto wawili mmoja ana miaka 19 na mwingine 11 alionao hawana mtu wa kuwasaidia kwa sababu tayari wameshampoteza mama yao, tunaomba mshtakiwa arudi nyumbani kwake ili awatunze watoto wake wasijione yatima.
Mapema, wakili wa Serikali, Justus Ndibalema alimsomea mshtakiwa kosa la lake linalomkabili akidai kuwa mshtakiwa alikuwa anaishi na mke wake Clara maeneo ya Keko mwanga wilayani Temeke jijini Darbes Salaam, na kwamba Januari 13,2016 majira ya jioni Clara alitembelewa na dada yake Veronika Munishi nyumbani kwake .
Amedai, akiwa hapo, Clara alimfahamisha dada yake huyo kuwa mume wake Kaberwa majira ya mchana alimpiga wakati huo mshtakiwa hayupo hapo nyumbani.
Baada ya hapo Clara na Veronika walienda dukani kununua mafuta ya kupikia wakati wanarudi nyumbani walimkuta mshtakiwa amerudi nyumbani ndipo ugomvi ulianza baina yao ambapo wakati ugomvi ukiendelea Veronika alifanikiwa kukimbia wakati mshtakiwa akiendelea kumpiga mdogo wake Clara huku akimburuza na kumtoa nje ya geti ndipo marehemu akapiga kelele na majirani wakaja.
Kabelwa alipowaona majirani hao alikimbia ambapo walimchukua Clara na kumpeleka kituo cha Polisi na baadaye walimkimbiza katika hospitali ya Rufaa ya Temeke.
Aliendelea kueleza kuwa, hali ya Clara iliendelea kuwa mbaya na ilipofika Januari 14,2016 alifariki na mwili wake ulipelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi.
Alidai kuwa, Januari 18,2016 uchunguzi wa mwili wa marehemu ulifanyika na ripoti ilionyesha sababu ya kifo chake damu ilivia tumboni.
Ilidaiwa kuwa, Januari 15,2016 Kabelwa alikamatwa eneo la Kilosa mkoani Morogoro na kuletwa kituo cha Polisi Chang'ombe.
Mhandisi wa kampuni ya Best World, Nivat Kaberwa akitolewa mahakamani tayari kwa kwenda kuanza kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukiri shtaka la kumuua mke wake
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...