Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
WATU 14  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kusambaza ujumbe usiohitajika kwenye mitandaoni pamoja na utakatishaji fedha.

Washitakiwa hao waliofikishwa mahakamani hapo jana ni David Simon, Michael Joseph, Omary Rajabu, Ramadhani Issah, Adolph Martine, Martine Maiko, Ajuaye Gerald.

Wengine ni Adam Christopher, Frank Magazi, Mathias Godfrey, Joseph Mabruck, John Mwambusa, Hamza Hassan , Amosi Mazwile.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali, Nancy Mushumbusi amedai mbele ya Hakimu Mwandamizi, Hamza Wanjahz kuwa katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2017 na Mei 31, mwaka huu, katika maeneo ya Sumbawanga mkoani Ruvuma na maeneo mengine tofauti ya Tanzania washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Pia washtakiwa kwa makusudi huku wakijua walisambaza taarifa za uongo kwa njia ya ujumbe mfupi kwa kutumia kompyuta kwa lengo la kudanganya umma.

Aidha, washitakiwa kwa pamoja walipanga kusambaza ujumbe usiohitajika kwenye mitandao  kwa njia ya kompyuta huku wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Katika shtaka la nne, washtakiwa wanadaiwa kujihusisha katika muamala unaohusu fedha taslimu  Sh. Milioni 11 wakati wakijua fedha hizo ni mazao ya kosa la jinai la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Hata hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchum.

Wakili Mushumbusi alidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo aliomba mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 7, mwaka huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...