*Wafungwa wamuomba Rais Magufuli dua maalum
*Ni baada ya kuamua kusikiliza changamto zao 
*Awaambia amepata soko kubwa na limemuingia 


Na Said Mwishehe-Michuzi TV

RAIS Dk.John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Butimba mkoani Mwanza ambapo amekiri  kuona na kuyasikia mengi, hivyo ameahidi kuyafanyia kazi.

Akiwa katika gereza la Butimba Rais Dk.Magufuli amepata nafasi ya kusikiliza changamoto mbalimbali za wafungwa ikiwemo ya kufungwa baada ya kubambikiziwa kesi, kuombwa rushwa, kesi kukaa muda mrefu pamoja na aina nyingine za malalamiko.

Wakati kwa upande wa Askari Magereza wa Butimba nao wameeleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo na kufafanua changamoto kubwa ni usafiri, nyumba za askari na kukosa mtaji wa kuendeleza mradi wao wa kokoto na mradi wa kuvua samaki.

Akizungumza baada ya kuwasikiliza wafungwa na askari magereza , Rais Magufuli amesema kufika kwake gerezani hapo kuna somo kubwa limemuingia na akwenda kulifanyia kazi.

"Niliyoyasikia lazima nifanyie kazi, nimesikia changamoto za wafungwa na nimesikia pia changamoto za askari wangu.Niahidi nitayafanyia kazi yote ambayo nimeyasikia kwenu wote,"amesema Rais Magufuli na kuongeza hayuko tayari kuona askari magereza wanalalamika wakati yeye yupo.

Rais Magufuli amefafanua kwenye gereza hilo la Butimba amegudua mambo mengi , amebaini kuna kuombwa rushwa wafungwa na mahabusu na uamuzi wake wa kufika hapo umetokana na kufahamu mambo mengi ambayo mengine wafungwa wameshindwa kueleza.

Amewahakikishia wafungwa hao kwamba amewalewa wafungwa na mahabusu hao na kuahidi kuwa amewasikia na yote ambayo ameleezwa yatafanyiwa kazi."Niahidi nimewasikia, nimewasikia na yote nitayafanyia kazi.Naomba muwe wavumilivu na niaminini."

Rais Magufuli amesema hata walioko uraiani ni wafungwa au mahabusu wabadae na kwamba kufungwa au kuwa mahabusu haina maana ya kukosa haki za kibinadamu.

"Ndio maana nimekuja hapa kuwasalimu, nimesikia changamoto zenu lakini wakati huo huo nimeona changamoto za askari wangu ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu.Pia nafahamu kuna watu wamefungwa kwa kubambikiziwa kesi, kuna watu kesi zao zinacheleweshwa kwasababu hawajazungumza na polisi.Nimeguswa na niliyoana hapa gereni,"amesema Rais Magufuli.

Wakati anazungumza gerezani hapo Rais Magufuli amewaomba wavumilie na kuwaeleza wafungwa amekwenda gerezani hapo na viongozi wa ngazi mbalimbali na kwamba nao wamesikia yaliyosemwa.

Baadhi ya wafungwa wametumia nafasi hiyo kumueleza Rais namna ambavyo wananyanyaswa na baadhi ya askari wa magereza huku wengine wakilalamikia kukaa muda mrefu bila kusi kusikilizwa.Pia wapo wafungwa ambao wamemuomba Rais Magufuli aangalie namna ya kuwasaidia ili watoke kwani wamejirekebisha na kuwa raia wema.

Kabla ya Rais kuondoka gerezani hapo, wafungwa na mahabusu wamefanya ombi maalumu ili Mwenyezi Mungu azidi kumpa baraka katika kulitumikia Taifa letu huku pia wakieleza kuwa wao wafungwa wameeleza kazi kubwa na nzuri anayoifanya, hivyo wametumia dua hiyo kuomba wale ambao hawajamuelewa Rais nao wamuelewe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...